Klabu ya
Coastal Union imefanya mkutano wake wa dharura leo na kuzika tofauti za
wanachama zilizokuwa zikiitafuna klabu hiyo.
Mkutano huo
uliofanyika mjini Tanga umeonyesha kuzaa matunda na sasa wanachama hao wameamua
kuunganisha nguvu kwa ajili ya kuisaidia klabu na timu yao.
Katika mkutano
huo, pamoja na masuala muhimu ya klabu, umoja na kushirikiana kwa pamoja, suala
la wanachama wapya pia lilijadiliwa. Pia wamekubaliana uchaguzi mkuu utafanyika Julai, mwaka huu.
Awali, uongozi
wa Coastal Union ulikataa kupokea maombi ya wanachama wapya kwa madai eti
wanataka kufanya vurugu.
Lakini katika
mkutano wa leo, wanachama wapya wamepewa nafasi kikubwa wanachotakiwa ni
kufuata utaratibu.
Baadhi ya
mashabiki waliamua kuunda kundi lao maalum baada ya kukataliwa kupewa uanachama
hali iliyooonyesha uongozi ulikuwa haujiamini na viongozi wake walikuwa na hofu
ya ushindani hasa kwa kuingiza wanachama wapya, vijana na wasomi.
0 COMMENTS:
Post a Comment