Simba imeamua
kuachana na Kocha Piet de Mol raia wa Ubelgiji ambaye ilielezwa atachukua
mikoba ya Goran Kopunovic.
Awali ilielezwa, De
Mol anatarajia kutua nchini kati ya Mei 21 hadi 23
tayari kumaliza na uongozi wa Simba na mara moja ataanza kazi.
Lakini taarifa
za uhakika zimeeleza tayari Simba imemuondoa De Mol katika kundi la makocha
inaowawania kuchukua nafasi ya Kopunovic.
“Simba sasa
haina mpango na kocha huyo, kuna makocha wengine watatu ndiyo tunaangalia
mmoja. Hivyo huyo De Mol wala hawezi kuja,” kilieleza chanzo cha uhakika.
Uongozi wa
Simba umefikia uamuzi huo baada ya Kopunovic kutaka dau kubwa sana.
Kopunovic
aliondoka mapema wiki hii kurejea kwao huku akiwa ameshindwa kuelewana na
uongozi wa Simba.
MSerbia huyo
anayeishi nchini Hungary alitaka kulipwa dola 50,000 (sh milioni 100) kama ada
ya usajili.
Pia alitaka
kupewa mshahara wa dola 14,000 ambazo zingemfanya kuwa kocha ghali zaidi
nchini.
Simba iliamua
kubadili uamuzi wa kubaki naye na kufanya mazungumzo na Mbelgiji huyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment