Uongozi wa Simba
haujaridhishwa na nafasi ya tatu iliyotwaa msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara,
hivyo umetenga Sh milioni 200 kwa usajili wa kikosi chake ili kitishe msimu
ujao.
Kati ya hizo, tayari Sh
milioni 30 zimeshatumika kwa kumuongezea mkataba kiungo wake Said Ndemla, hivyo
sasa zimebaki Sh milioni 170.
Simba ilipanga pia kumpa
mkataba mpya winga wake, Ramadhan Singano kwa dau la Sh milioni 30 lakini
mwenyewe amezikataa akitaka apewe Sh milioni 50 taslimu.
Mmoja wa watu muhimu
katika Kamati ya Utendaji ya Simba na Kamati ya Usajili, amesema kiasi hicho
cha fedha kitatumika kwa ajili ya kusajili wachezaji makini watatu hadi wanne
ili kuimarisha kikosi chao msimu ujao.
Chanzo hicho kilisema,
kati ya wachezaji hao wamepanga kusajili mshambuliaji mmoja kutoka Burundi na
wengine wazawa waliowaona kwenye usajili wa msimu huu.
“Katika msimu huu
hatutaki kutumia fedha nyingi za usajili, tumeona hakuna haja kwa sababu timu
haishiriki michuano migumu ya kimataifa.
“Tumetenga Sh
milioni 200 kwa ajili ya kusajili wachezaji kati ya watatu hadi wanne
tutakaowatumia kwa ajili ya msimu ujao wa ligi,” kilisema chanzo hicho.
Mwenyekiti wa Kamati ya
Usajili ya Simba, Zakaria Hans Poppe, ameliambia Championi Jumamosi: “Tutasajili
wachezaji watatu tu wenye uwezo, hatutasajili wachezaji wengi kwa ajili ya
msimu ujao. Kati ya wachezaji tutakaowasajili, mmoja atakuwa ni mshambuliaji wa
kigeni.”
0 COMMENTS:
Post a Comment