Kocha Mkuu wa Taifa
Stars, Mart Nooij amesema Taifa Stars ilifanya kila kinachowezekana kushinda dhidi ya Swaziland, lakini bahati haikuwa yao.
Akihojiwa na runinga ya SuperSport mara baada ya mechi hiyo ya kwanza ya Kombe la Cosafa, Nooij alisema Stars ilishambulia zaidi lakini tatizo lilikuwa katika kupata bao.
"Tulicheza vizuri zaidi, tulipata nafasi zaidi lakini tulishindwa kupata bao la kusawazisha.
"Lengo lilikuwa angalau kusawazisha, lakini utaona hatukuweza kufanikiwa na utaona wenzetu wametumia nafasi moja tu waliyipata," alisema.
Stars imeanza michuano ya Cosafa kwa kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Swaziland.
Huwa hatukosi la kusema,lakini wengi tunajua kwamba Tanzania Mara nyingi ni wasindilizaji tu.
ReplyDelete