May 18, 2015


Taifa Stars imeanza michuano ya Cosafa kwa kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Swaziland.

Swaziland ambao hawakuwa wa kutisha sana wameifunga Stars kwa bao hilo moja katika mchezo ambao ulikuwa na kazi.

Swaziland walipata bao la kuongoza kwa bao la Simbizo Mabila beki wa kulia wa Swaziland aliyefunga katika dakika ya 43 baada ya kumchambua kipa Deogratius Munish ‘Dida’.

Stars walionekana kufanya juhudi za kusawazisha lakini Mrisho Ngassa, John Bocco na Simon Msuva walipoteza nafasi nzuri walizozipata katika kipindi cha kwanza.

Katika kipindi cha kwanza, Taifa Stars imefika langoni mwa Swaziland mara 11 wakati wapinzani wao wamefika mara nane.

Hadi mwisho wa dakika 45 Swaziland wamemiliki mpira zaidi kwa 54% wakati Stars wana 46%.

Mechi ijayo Stars itacheza Mei 22 dhidi ya Lesotho na inahitaji kushinda ili kuamsha matumaini ya kuvuka katika kundi B.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic