Uongozi wa Mbeya City umefunguka kuwa, katika
moja ya changamoto walizokumbana nazo msimu huu ni pamoja na kupata mapato
kidogo, tofauti na msimu uliopita na hii ni kutakana na mfumo ule wa
kielektroniki pamoja na aina ya viwanja ambavyo walikuwa wakitumia huku leo
wakitarajiwa kupokea ripoti ya kocha wao.
Mbeya City msimu uliopita ilimaliza nafasi ya tatu na kuwa
moja ya timu ambazo zilijikusanyia mapato mengi, nyuma ya Simba na Yanga
kutokana na kujizolea mashabiki wengi, japo ulikuwa msimu wao wa kwanza ligi kuu.
Mwenyekiti wa timu hiyo,
Mussa Mapunda, alisema wamepitia changamoto nyingi lakini kubwa ikiwa ya
mapato.
Mapunda alisema TFF na Bodi ya Ligi,
wanatakiwa kujipanga upya na kuwa makini katika hilo, kwani licha ya mfumo ya
kielektroniki kusimamishwa lakini mapato yawekuwa madogo kutokana na hata aina
ya viwanja ambavyo wamekuwa wakitumia.
“Mapato ya msimu huu naweza sema ni kiduchu,
si kama msimu uliopita na hii ilichangiwa na mambo kadhaa, la kwanza, mwanzo
tulianza kutumia tiketi za kielektroniki lakini pia tumekuwa hatuvuni mapato
katika baadhi ya viwanja kama Mabatini, Pwani na Manungu, Turiani.
“Na hii ni kutokana na kuwa na mashabiki
wachache, unakuta timu inaambulia kama laki mbili, hata ukiwapa wachezaji
wanashindwa kugawana, pia kingine ni uwezo wa Azam TV, mashabiki wengi wamekuwa
hawaendi viwanjani, zaidi wanaangalia kwenye runinga,” alisema Mapunda.
0 COMMENTS:
Post a Comment