Kocha wa zamani wa Yanga, Kostadin Papic ameongeza
miaka miwili ya kuendelea kuifundisha timu ya Polokwane City ya Afrika Kusini.
Papic ,54, ameongeza mkataba huo ikiwa ni siku
chache baada ya kuteuliwa kuwa mmoja wa makocha wanaowania tuzo ya Makocha Bora
wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini (PSL).
Papic
raia wa Serbia aliinoa Yanga misimu minne iliyopita kabla ya kuondoka na kwenda
zake Afrika Kusini.
0 COMMENTS:
Post a Comment