MAVUGO (KUSHOTO) AKIWA KAZINI NCHINI RWANDA... |
Wakongwe Simba wana tatizo
katika safu yake ya ushambuliaji. Sasa wameanza harakati za kusajili straika wa
maana ili aifungie mabao msimu ujao na sasa ipo katika mazungumzo na
mshambuliaji wa Kiyovu SC ya Rwanda, Laudit Mavugo raia wa Burundi.
Kocha wa Simba, Goran
Kopunovic ndiye aliyepeleka jina la Mavugo kwa Kamati ya Usajili ya timu hiyo
ili asajiliwe baada ya Dan Sserunkuma kuondoka kikosini.
Mmoja wa mabosi wa kamati
ya usajili amesema , Mavugo anaelezwa kuwa na uwezo
unaofanana na Amissi Tambwe wa Yanga ambaye pia ni raia wa Burundi kama yeye.
Alisema tayari Kopunonic
ambaye hatma yake ipo shakani Simba, ameshawasiliana mara kadhaa na Mavugo
mwenye umri wa miaka 25 ili aje kumaliza tatizo la ufungaji mabao klabuni hapo.
“Kuna straika
alianza mazungumzo na uongozi baada ya Kopunovic kuweka wazi sifa zake,
anatokea Burundi na aliwahi kufanya kazi katika timu ya Polisi ya Rwanda,”
alisema.
Mavugo aliyewahi
kuichezea Vital’O ya Burundi alilazimika kuondoka Polisi ya Rwanda baada ya
kuibuka kwa sheria mpya ya kupunguza idadi ya wachezaji wageni. Hata hivyo
kusajiliwa kwake Simba kutategemea na uwepo wa Kopunovic kikosini.
0 COMMENTS:
Post a Comment