Simba inaendelea na usajili wa kimataifa
lakini imepanga kuzunguka na kufanya utafiti kwa nchi tano hapa Afrika huku
lengo likiwa ni kumtafuta straika mmoja tu atakayekuja kuziba pengo la Mganda,
Dan Sserunkuma.
Simba imepanga kufanya usajili huo kwa kuwa
tayari inaye straika mwingine atakayejiunga na timu hiyo msimu ujao, Mkenya,
Paul Kiongera, anayetokea KCB ya Kenya alikokuwa akicheza kwa mkopo na
kuimarisha kiwango chake baada ya kukaa nje kwa muda mrefu akiuguza majeraha
aliyokuwa nayo baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, amesema nchi walizopanga
kwenda kuangalia mchezaji wa nafasi hiyo ni pamoja na Burundi, Kenya, Senegal,
Ghana na Uganda.
“Tunaamini tunaweza kupata straika mzuri
mwenye uwezo wa juu katika nchi tano ambazo tuna imani nazo katika nafasi hiyo,
tunaangalia katika nchi za Burundi, Kenya, Senegal, Ghana na Uganda.
"Lengo ni
straika mmoja, tukimaliza hapo tutakuwa na wachezaji wageni wanne na hiyo
nafasi moja tutaangalia kama kutakuwa na usajili wa nafasi yoyote ya lazima,”
alisema Hans Poppe.
Simba imeamua kuachana na Waganda wawili,
Simon Sserunkuma na Dan Sserunkuma na sasa imebaki na Emmanuel Okwi, Juuko
Murshid na Mkenya, Kiongera anayerejea.
0 COMMENTS:
Post a Comment