Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF), limetuma salamu za rambirambi kwa Chama cha Soka
Mkoa wa Rukwa (RUREFA) kufuatia kifo cha katibu mkuu msataafu wa chama hicho
Adolph Choma aliyefariki jumamosi na kuzikwa jana.
Katika salamu
hizo, TFF imesema inawapa pole familia ya marehemu Adolph Choma, ndugu jamaa na
marafiki, wapenzi na wadau wa mpira wa miguu nchini na kusema TFF ipo pamoja
nao katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.
0 COMMENTS:
Post a Comment