Siku chache baada ya kipa wa Yanga, Ally Mustapha ‘Barthez’ kuibiwa
gari, wezi wamevamia nyumbani kwa kipa nyota wa zamani wa Simba, Juma Kaseja.
Watu hao walivamia usiku nyumbani kwa Kaseja eneo la Mbezi kwa
Msuguri jijini Dar es Salaam na mmoja wao alifanikiwa kuingia hadi ndani baada
ya kuvunja vioo na kukata nondo.
Akiwa ndani, mwizi huyo alifanikiwa kung’oa televisheni na kuivusha
dirishani, pia akachukua vitu kadhaa vya umeme.
“Bahati nzuri Kaseja alishtuka, alipotoka nje aligundua kuna
uvamizi. Akaanza kuwasaka, mwisho wezi waligundua ameamka. Yule aliyekuwa ndani
alikimbia na kuruka ukuta.
“Jirani kwa Kaseja kuna askari pale alilazimika kupiga risasi ya
moto na kufanya wezi hao wakimbie kama wendawazimu,” alieleza Abubakar Salum ‘Sure
Boy’ ambaye ni jirani wa Kaseja.
“Taarifa zaidi muulize yeye mwenyewe Kaseja maana mimi nilienda kama
jirani tu ila, wengi walijua mimi ndiyo nimevamiwa kama ambavyo wewe
ulivyoniuliza.
Ingawa Kaseja hakupatikana, lakini taarifa zinaeleza hakuna
kilichoporwa isipokuwa uharibu uliofanywa na wezi hao wakati wakijaribu kusaka
njia ya kuingia ndani. Imeelezwa tukio hilo lilitoa saa 10 alfajiri, usiku wa
kuamkia juzi.







0 COMMENTS:
Post a Comment