Rais wa Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amewaagiza wasimamizi wa vituo vya
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuhakikisha sheria na taratibu zote za mechi
zinafuatwa.
Ligi Kuu ya Vodacom
(VPL) msimu huu 2014/2015 inafikia tamati kesho (Mei 9, 2015) ambapo timu zote
14 zitakuwa viwanjani katika mechi ambazo ndizo zitakazotoa hatma ya timu
zinazoshuka daraja.
Mechi hizo zitakuwa
kati ya Ndanda na Yanga (Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara), JKT Ruvu na
Simba (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam), Azam na Mgambo Shooting (Azam Complex,
Dar es Salaam), Stand United na Ruvu Shooting (Uwanja wa Kambarage, Shinyanga),
Kagera Sugar na Tanzania Prisons (Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza), Mbeya City na
Polisi Morogoro (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya), na Mtibwa Sugar na
Coastal Union (Uwanja wa Manungu, Morogoro).







0 COMMENTS:
Post a Comment