![]() |
Unaweza kusema
soka linalipa aluu! Maana magwiji wa zamani, Ryan Giggs na Garry Neville
wanamiliki hoteli maarufu karibu kabisa na uwanja wa Old Trafford.
Pamoja na
wao, wengine wenye hisa za umiliki ni Phil Nevile na Paul Scholes. Inajulikana kama
Hotel Footballl.
Imeelezwa inaingiza
faida kubwa na hata uongozi wa Manchester United umekuwa na mpango wa kuinunua.
Faida nzuri
ambayo wamekuwa wakipata, magwiji hao wa Man United wako katika hatua za mwisho
kutaka kufungua hoteli nyingine karibu kabisa na Uwanja wa Etihad unaomilikiwa
na Manchester City. Soka linalipa ukiwa makini.





















0 COMMENTS:
Post a Comment