Kocha Mkuu wa Kagera, Mbwana Makata,
ameshindwa kuvumilia maneno ya watu wanaobeza Tuzo ya Kocha Bora wa Msimu aliyochukua
wiki iliyopita kwa kusema kuwa kocha bora si lazima atwae ubingwa.
Mataka alijinyakulia tuzo hiyo mbele ya
makocha, Hans van Der Pluijm wa Yanga na Goran Kopunovic wa Simba ambao
walikuwa kwenye kinyang’anyiro hicho.
kocha huyo ambaye amejiunga na Kagera Sugar,
alifunguka kuwa tuzo yake ilikuwa sahihi kwani bila yeye Prisons ingeshuka
daraja.
“Nashukuru wote waliotambua kazi yangu
ambayo binafsi nilikuwa shujaa. Niliikuta timu kwenye wakati mgumu sana,
ilikuwa mkiani na pointi 13, kwa tofauti ya pointi 12, nyuma ya timu ya pili
kutoka chini.
“Kila mmoja alikuwa akiniuliza kama ningeweza
kuisaidia, lakini niliwajibu kuwa mimi ni daktari sina haja ya kuogopa hali ya
mgonjwa. Nilipigana hadi ikabaki,” alisema Makata na kubeza kiaina ubingwa wa
Yanga.
“Suala la kocha bora siyo lazima achukue
ubingwa. Mbona England, Chelsea ilichukua ubingwa tena mapema sana, lakini
kocha bora akachaguliwa wa Southampton (Ronald Koeman)? Kikubwa ni mchango wa
mtu kwenye timu na si kigezo cha ubingwa.”







0 COMMENTS:
Post a Comment