HANS POPPE |
Ingawa Simba wamekuwa wakiendelea kufanya siri lakini habari za ndani kutoka katika klabu hiyo zinaeleza kocha wake atatokea nchini Uingereza.
Kama kweli watamalizana naye na kuwa na kocha kutoka Uingereza, basi Simba wataungana na Azam FC ambayo imemrejesha Stewart Hall ambaye pia ni raia wa Uingereza.
Taarifa zimeeleza makocha wengi waliofanya majadiliano na Simba, lakini inaonekana kocha Mwingereza ndiye ameonekana kuwavutia zaidi.
Ingawa vyombo vingi vya habari viliripoti kuhusiana na kocha kutoka Ufaransa, taarifa za uhakika zinasema kocha huyo mpya wa Simba atatokea, Uingereza.
Mwenyekiti wa Usajili wa Simba, Zacharia Hans Poppe, naye alikuwa kati ya waliosimamia msimamo wa Simba, kuhakikisha siri inaendelea kusimama, lakini akakubali kuwa anatokea Uongereza.
"Mmeshindwa kuwa na subira, lakini kweli atatokea Uingereza. Vuteni subira, baada ya kuuangalia mkataba, akikubali na kusaini, basi tutawatangazia," alisema Hans Poppe.
Simba ililazimika kuanza kusaka kocha mpya baada ya Goran Kopunovic kudai dau kubwa la Sh milioni 100 ili asaini mkataba wa miaka miwili.
Jambo hilo limeonekana kuwakera viongozi wengi wa Simba na kuona Mserbia huyo ana tamaa. Hivyo, mara moja wakaanza kazi ya kutafuta kocha mpya.
kocha toka Uingerza?.....hapa SIMBA tunabugi,kwa nini tusimrudishe Kuponovic aliyekubali kushusha dau au ifanyike jitahada ya kumrejesha Milovan Circovic,Nawaambia viongozi wetu huyo muingeraliieza atakuja kama Mtalii
ReplyDelete