Siku mbili tu baada ya kutwaa ubingwa wa Ulaya,
Barcelona imeendelea na usajili baada ya kumnasa beki Aleix Vidal kutoka
Sevilla.
Sevilla ambao ni mabingwa wa Europa, wamekubali
kumuachia beki huyo mwenye miaka 25, hata hivyo atalazimika kusubiri hadi
Januari, mwakani kuichezea timu yake mpya.
Barcelona bado inatumikia adhabu ya Fifa ya usajili
hadi mwakani. Hivyo Vidal atakuwa pamoja na timu hiyo, lakini ataonekana
uwanjani na Barcelona, mwakani.
WAKATI AKIWA NA SEVILLA. |
0 COMMENTS:
Post a Comment