June 26, 2015

SALIM (ALIYEVAA FULANA YA ADIDAS, AKIWA NA MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI YA SIMBA, SAID TULLY ALIYEKWENDA KUMPOKEA.

Kocha mpya wa makipa wa Simba, Iddi Salim raia wa Kenya amewasili jijini Dar es Salaam.

Salim amewasili leo mchana ili kumalizia mazungumzo na Simba.

“Nafika hapa kwa ajili ya kumalizia mazungumzo na Simba. Niko tayari kufanya nao kazi baada ya kufikia makubaliano,” alisema kocha huyo wa zamani wa Gor Mahia.

Salim kwa sasa ni kocha wa AFC Leopards ya Kenya na pia amekuwa mmoja wa makocha bora wa makipa kwa Afrika Mashariki.


Amewahi kuwa kocha makipa wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars akiwa chini ya Kocha Adel Amrouche raia wa Ubelgiji mwenye asili ya Algeria.

1 COMMENTS:

  1. Kwanini tusiige utaratibu wa wazungu!? kocha mkuu anakuja na benchi lake la ufundi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic