June 16, 2015


Na Said Msumi
Safari ya kuelekea mashindano ya mataifa huru ya Afrika (CAN) mwaka 2017 nchini Gabon imeanza june 12 ambapo Tanzania ilitupa karata yake ya kwanza   Juni 14 dhidi ya timu ya taifa ya Misri ’Mafarao’  ambapo katika mchezo huo Taifa Stars ilikubali kichapo cha mabao 3-0, yaliyofungwa na Mohamed Salah, Basem Morsi na Rami Rabia. Katika makala yangu mnamo Desemba 12, kichwa cha habari kilikuwa "Naanza kuchagua timu yangu ya Afcon sasa".


Niliezea kuhusu  ushiriki wa timu ya taifa ya Tanzania taifa stars kuhusu mashindano yanayokuja kwa mwaka 2017 hasa nikigusia upande wa wachezaji,viongozi na mashabiki kwa ujumla.Lakini hebu tuangazie mambo kadhaa tunaopaswa kuyaangalia katika mbio zetu kuelekea mashindano haya ya CAN.

Rekodi
Timu ya taifa ya Misri inashika nafasi ya 55 katika viwango vya mpira duniani(FIFA) kabla ya mchezo wa jumapili tumekutana mara nane huku tukipoteza michezo saba na kutoka sare mchezo mmoja.Wadau wengi wamekuwa hawaamini kwenye upande wa rekodi lakini bado timu hii ya misri ni kikwazo kwetu na tusipo angalia tunaweza tukapoteza hata mchezo wa nyumbani.
05 Jun 1975
Tanzania vs Egpty
1-1
01 Aug 1975
Egpty  vs Tanzania
5-2
12 Mar 1980
Egpty  vs Tanzania
2-1
04 Apr 1987
Tanzania vs Egpty
2-4
17 Apr  1987
Egpty  vs Tanzania
6-0
14 Oct 1994
Egpty  vs Tanzania
5-1
22 Apr 1995
Tanzania  vs Egpty
1-2
05 Nov 2009
Egpty  vs Tanzania
5-1
05 Jan  2011
Egpty  vs Tanzania
5-1

Nigeria
Timu ya  taifa ya Nigeria’super eagles’ yenyewe inashika nafasi ya 43 katika viwango vya FIFA  ambapo yenyewe katika  kundi G inashika nafasi ya pili baada ya ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Chad. Bado rekodi yetu dhidi ya wababe hawa Afrika sio nzuri hata kidogo hasa ikumbukwe mchezo unaofatia tunacheza nao nyumbani  mnamo September.

06 Jul 1972
Tanzania  vs Nigeria
0-0
12 Jan 1973
Nigeria  vs   Tanzania
2-1
08 march 1980
Nigeria vs   Tanzania
3-1
06 Dec 1980
Nigeria vs   Tanzania
1-1
20 Dec 1980
Tanzania  vs Nigeria
0-2
11 sept 2002
Nigeria   vs     Tanzania
2-0

Chad
Timu hii taifa ya Chad ndio inaonekana kama kibonde katika kundi hili ambapo katika  viwango  vya FIFA timu hii inashika nafasi ya 172 ambapo ipo chini ya Tanzania  lakini katika michezo miwili tulikutana nao tumeweza kuwafunga kwao  magoli 2-1 lakini na wao walitufunga 1-0 lakini si timu ya kubeza hata kidogo katika mashindano haya. Yenyewe inashika nafasi ya tatu  katika kundi letu kutokana na kufungwa magoli machache dhidi yetu.
                                                 

TFF
Shirikisho la mpira la Tanzania(TFF) nadhani wao kwa upande wao wamefanya kila kitu kwa wachezaji na benchi la ufundi kwa sababu mosi wameiweka timu kambini zaidi ya wiki mbili huko Ethiopia lakini pili timu hii iliweza kushiriki katika mashindano ya Cosafa ili kuipa timu mechi nyingi za kirafiki lakini ingawaje tulikosa mechi ya kirafiki katika kalenda ya Fifa lakini TFF kupitia kamati zake za ufundi hasa mkurugenzi wa ufundi ambaye anahusika na uteuzi wa wachezaji wa timu ya taifa kwa kushirikiana na kocha mkuu wanaweza wakapewa lawama kutokana na uchaguzi wa wachezaji.

Swali la kujiuliza mkurugenzi haoni wachezaji mbadala kwa baadhi ya wachezaji ambao hawafanyi vizuri katika timu ya taifa?

Kocha
Kocha Mkuu, Mart Nooij ameonekana kama hafai kuendelea kuifundisha timu yetu ya taifa  lakini suala la kujiuliza wachezaji wetu wana ubora wa kupambana na wachezaji kariba ya wamisri au Nigeria?

Kwa hapa hatupaswi kumlaumu kocha lakini jambo ambalo kocha anapaswa kulaumiwa ni uteuzi wa kikosi jambo ambalo alipingwa toka  awali tangia michuano ya Cosafa, si nia yangu kuwapigia chapuo baadhi ya wachezaji lakini uwezo wao  ulishahili wawepo kikosini wachezaji kama Mohamed Husein ‘Tshabalala au Ally Mustapha ‘Barthez’ walitakiwa kuwa katika timu ya taifa nadhani hapa kocha anapaswa kulaumiwa.

Lakini pia hata rekodi za mechi alizoziongoza sio nzuri hata kidogo hapa anapaswa kupewa  lawama pamoja na benchi lake la ufundi kwa ujumla.

Wachezaji
Ukirejea kwenye makala yangu nilitoa ushauri kwa wachezaji wetu kutambua thamani ya jezi ya taifa pindi wanapovaa jezi hiyo nadhani wachezaji wanapaswa kucheza zaidi ya uwezo wao mathalani mchezo dhidi ya Cameroun kwao mjini Younde tuliopeteza kwa mabao 2-1 au dhidi ya Burkina Faso katika mji wa Ouagaduoguo tulioshinda bao1-0 au tuliopoteza dhidi ya Ivory Coast kwao mabao 2-0.

Hata kama tulipoteza kila mtu alihamasika na kiwango cha wachezaji nadhani wachezaji wanapaswa kubadilika kwa sababu wao ndio wenye jukumu la kuleta mafanikio na sio kocha.

Nadhani sasa ni wakati mzuri kwa TFF kuwashirikisha wachezaji wa zamani katika timu ya taifa ilikuwasaidia kuwapa ujuzi zaidi mana sasa mchezaji wa zamani ni mmoja tu ambaye naye ni meneja Tasso Mukebezi lakini pia serikali,wadau muda ni sasa kujipanga mapema  mana mechi dhidi yetu na Nigeria sio mbali maandalizi ya uhakika yanahitajika mapema na sio kuwatupia lawama baadhi ya wachezaji kama Oscar Joshua na wengineo.

Mwandishi wa makala hii ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Shahada ya Mahusiano kwa umma- UDSM

0654-234573

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic