Mshambuliaji mkongwe Gaudence MWaikimba
ametua JKT Ruvu iliyopania kujiimarisha ili ifanye vizuri msimu ujao.
Mwaikimba aliyekuwa akikipiga Azam FC,
amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea JKT Ruvu.
Mbele ya Makamu Mwenyekiti wa JKT, Meja
Hassan Mabena Mwaikimba amemwaga wino, tayari kwa msimu ujao.
Tayari JKT imefanikiwa kumsainisha mshambuliaji
Saad Kipanga kutoka Mbeya City.
JKT wamepania kukiboresha kikosi chao
ili kufanya vizuri zaidi msimu ujao.









0 COMMENTS:
Post a Comment