Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi
na Teknolojia, January Makamba ametangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania
kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Makamba aliyejieleza vizuri kwa kufafanua
masuala mengi, pia amezungumzia michezo na kusema atahakikishia anajenga vituo
vya Kiolimpiki.
Pamoja na vituo hivyo, Makamba ambaye
ni Mbunge wa Bumbuli, amesema atahakikishaa najenga vitu vya watoto wenye
vipaji.
“Lazima kuwe na vituo ambavyo
vitaendeleza vipaji vya watoto ambao wanaonekana kuwa na vipaji.
“Lengo ni kurudisha kizazi kipya
chenye wanamichezo mahiri,” alisema na kuongeza.
“Nitarudisha michezo mashuleni maana
ndiyo sehemu ambayo serikali inakutana
na watu wake wengi kwa wakati mmoja, hivyo ni lahisi kuwatengeneza.”
Makamba viongozi wa michezo nao
watalazimika kuwajibika na wanayoyafanya huku akishangazwa kuwa watu wengi
maarufu kama magumashi, yaani wasio makini hukimbilia kwenye michezo.
“Nimeambiwa watu wengi magumashi,
wanakimbilia michezoni. Jambo ambalo litaisha, lazima wawajibike. Pia
nitapambana kutengeneza miundombinu ili kuendelea kusaidia kukua kwa michezo,”
alisema.
Makamba ni kati ya wagombea waliojitokeza
wenye umri mdogo zaidi.
Hotuba yake imeelezwa kuwa moja ya
zile bora kwa wagombea waliojitokeza kuwania urais kupitia CCM.
0 COMMENTS:
Post a Comment