Mmoja wa makada wa CCM
aliyetangaza nia ya kugombea Urais, Bernad Membe amesema ataendelea kuijali
michezo,wanamichezo wenyewe pamoja na sanaa.
Membe ambaye ni Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, amesema atahakikisha kunakuwa na
wanamichezo wanaopelekwa nje.
“Tutaendelea kuwapeleka
wanamichezo nje kwa ajili ya kujifunza kwa ajili ya kujenga timu zetu imara.
“Vyuo vilivyo hapa
nyumbani pia vitapewa nguvu kuhakikisha vinatoa msaada kusaidia wanamichezo,”
alisema Membe.
Membe ni ambaye amekuwa
akishiriki katika masuala ya michezo na pia sanaa mara kadhaa, ni kati ya
wanaopewa nafasi kunyakua nafasi hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment