Mshambuliaji mkongwe aliyejiunga na Simba, Mussa Mgosi anapenda
kuvaa jezi namba 11 katika timu yoyote anayojiunga nayo, hata hivyo sasa hana
jinsi kwani na kusema kuwa angependelea sana kupewa namba 17 ambayo ilikuwa ya Amissi Tambwe
aliyetimkia Yanga.
Mgosi amesajiliwa na Simba baada ya kumaliza mkataba wake na
Mtibwa Sugar na tayari ameanza mazoezi na timu yake mpya.
Mgosi ambaye anarejea Simba baada ya kuitumikia miaka ya hivi
karibuni, alisema huwa anapenda kuvaa jezi namba 11 lakini sasa ina mtu
(Ramadhan Singano ‘Messi’) hivyo angependa apewe ya Tambwe, ikishindikana zaidi
akabidhiwe namba 10, iliyokuwa na Shabaan Kisiga ‘Marlone’.
“Siku zote huwa navaa jezi namba 11, hata Mtibwa nilikuwa navaa
jezi hiyo lakini nimekuja Simba nimekuta hiyo jezi anavaa Messi na haitakuwa
vizuri kumnyang’anya.
“Badala yake nitavaa namba 17, ikishindikana kabisa nitava 10 kwani
ndilo chaguo langu la pili baada ya namba 11, lakini haya yote yatategemea na
uwepo wa hiyo namba kwani nimekuja Simba zaidi kucheza mpira siyo kuchagua
namba ya jezi,” alisema Mgosi.
Jezi namba 11 kwa sasa inavaliwa na Messi ambaye yupo katika matatizo
ya mkataba wa usajili na Simba lakini namba 17 iliachwa na Amissi Tambwe ambaye
alijiunga na Yanga Desemba mwaka jana.
Mgosi ameanza mazoezi ya gym na Simba jijini Dar es Salaam kujiandaa
na msimu ujao wa Ligi Kuu Bara utakaoanza baadaye mwaka huu.
Kwa upande wa beki Haji Nuhu amesema angependa kupewa namba 38,
kiungo Peter Mwalyianzi anasema yake ni namba 3 (inavaliwa na William Lucian
‘Gallas’) kwa kile alichosema ni kukubali soka la Haruna Moshi ‘Boban’ huku
Mohammed Fakhi akisema yake namba 26 tayari inatumiwa na nahodha Hassan
Isihaka, hivyo atachukuwa yoyote.
0 COMMENTS:
Post a Comment