June 30, 2015

MURO
Mkurugenzi wa Kitengo cha habari cha Yanga, Jerry Muro amevunja ukimya na kujibu dongo la Haji Manara wa Simba kwa kusema Yanga wanajiamini.


Muro amemjibu Manara ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Simba kwa kumuambia Yanga si wachawi, hivyo hawana sababu ya kufanya mambo yao kwa kificho.
 
MANARAManara alikaririwa akijitapa jana kwamba Simba inafanya mambo yake kwa uficho mkubwa, si kama wenzao (Yanga) ambao kila kitu chao kipo kwenye vyombo vya habari.

“Tuna haja gani ya kuficha, wachezaji wawili kutoka Ghana na Zimbabwe wamekuja, tumewafanyia vipimo na mwisho wameingia mkataba.
“Hatuna sababu ya kuficha jambo, tunajiamini. Sisi si wachawi kufanya mambo kificho. Wenzetu huenda hawana fedha.

“Au inawezekana usajili wao una mambo ya figisufiisu, hivyo wanataka kuficha,” alisema Muro.


Yanga imefanikiwa kuwasajili Donald Ngoma na Joseph Zuttah ‘Tetteh” kutoka Ghana na kukamilisha idadi ya wachezaji saba wa kulipwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic