June 22, 2015


USAJILI wa Bongo una mengi na kila mmoja ana maamuzi yake. Kiungo mshambuliaji Haruna Moshi ‘Boban’ amekaa chini na kukubali kumaliza dili na viongozi wa Mbeya City huku akikataa kutua Mwadui kwa dau nono.

Iko hivi, Boban aliyewahi kuichezea Simba kwa mafanikio makubwa, mapema aliitwa na Mbeya City kwa ajili ya kumsajili kuichezea timu hiyo msimu ujao lakini wakashindwana kwenye masuala ya maslahi ambapo ilifafanuliwa kwamba Boban alitaka zaidi ya Sh milioni 10 kama ada ya usajili na City walikuwa tayari kumpa Sh milioni sita pekee. 

Hata hivyo, baadaye wakazungumza tena ‘kiutu-uzima’ na mambo yakakaa sawa, wakakubaliana kwamba atatua klabuni hapo kwa dau la Sh milioni 8 ili akakiongezee nguvu kikosi hicho chenye wachezaji nyota kama Juma Nyosso, Steven Mazanda, Themi Felix, Mwegane Yeya na wengine wengi.

Lakini wakati Boban akisubiri fedha hizo ili amwage wino City, ghafla Mwadui FC ya Shinyanga yenye wachezaji mastaa wa kutosha, ikamuibukia na kutaka kumalizana naye ila kabla hata ya majadiliano, Boban akaweka msimamo wake na kuwachomolea vigogo hao licha ya kuelezwa kuja na dau kubwa la kumnasa.

Mtu wa karibu na mchezaji huyo amesema,  Boban amekataa ofa ya Mwadui kwa sababu zake nyingi binafsi ambazo hakuwa tayari kumjuza mtu mwingine ingawa inaelezwa kuwa wingi wa mastaa waliosheheni Mwadui ndiyo kikwazo cha mchezaji huyo kukubali kuitumikia timu hiyo msimu ujao.

“Mbona fresh, Boban ameshamalizana na City kila kitu, sasa hivi anawasikilizia wamtumie fedha yake ya usajili ili atie saini lakini Mwadui nao walimtaka ila kawachomolea pamoja ya kwamba walikuja na pesa nzuri na mwenyewe Boban amesema kwamba hataenda Mwadui hata wampe milioni 50.

“Kikwazo kikubwa ni kwamba kule kuna mastaa wengi ambao Boban anahisi kutakuwa hakuna mpira wa kazi, wengi watakuwa wanaangalia majina yao, kwa hiyo kaona bora aende City akapige mpira na watu wa kazi kweli,” kilisema chanzo hicho kwa sharti la kutotajwa jina gazetini.

Kitu cha msingi baada ya hapo ilikuwa ni kutafutwa kwa Boban ili kujua zaidi kuhusu ishu hiyo lakini kupitia simu yake ya mkononi, akasema hivi kwa kifupi: “Saa hizi nimelala, nimepumzika kidogo, nicheki baadaye kama vipi.”

SOURCE: BOBAN

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic