Kocha Mkuu wa JKT Ruvu, Fred Felix Minziro,
amefunguka kuwa, licha ya wadau kusema mshambuliaji wake Gaudence Mwaikimba
umri umekwenda, watu watamshangaa atakapong’aa chini yake msimu ujao.
Mwaikimba ambaye ni mchezaji mkongwe aliyewahi
kuichezea Yanga misimu kadhaa hapo nyuma, alitemwa na Azam FC hivi karibuni
baada ya kuitumikia kwa miaka miwili.
Minziro alisema kuwa usajili wa Mwaikimba
katika kikosi chake utamaliza tatizo la ushambuliaji kutokana na kuwa butu na
kudai kuwa kiwango cha mchezaji huyo kilibadilika na kuwa bora katika kipindi
cha mwisho wa msimu wa ligi.
“Mwaikimba ni mchezaji mzuri na nina imani
kuwa nikiwa naye atarudi katika kiwango chake cha zamani kama ilivyokuwa Yanga
na timu nyingine kwani ni mchezaji mwenye kiwango kizuri, ndyio maana
nimemsajili.
“Kama utakumbuka mwishoni mwa ligi alionyesha
kiwango kizuri sana licha ya hapo nyuma hakuwa vizuri lakini naamini
atabadilika na kuwa tishio,” alisema Minziro ambaye timu yake ilimaliza katika
nafasi ya nane msimu uliopita.
0 COMMENTS:
Post a Comment