June 10, 2015

Hatimaye Newcastle United imefanikiwa kumpata kocha mpya kwa ajili ya msimu ujao.


Steve McClaren ndiye kocha mpya wa Newcastle ambayo inajivunia kwa kuwa mara mbili huko nyuma, kocha huyo aliwahi kukataa kuinoa.

McClaren ,54, kocha wa zamani wa England ameingia mkataba wa miaka mitatu kuifundisha timu hiyo.

Newcastle haikuwa na msimu mzuri baada ya kuboronga mechi nyingi hadi kuingia katika tishio la kuporomoka daraja.


Kitu kingine kizuri, McClaren  ameingia kwenye bodi ya Wakurugenzi wa Newcastle na kuwa kocha pekee katika ligi hiyo kuwa mmoja wa wanabodi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic