June 11, 2015

 Kikosi cha Yanga kinaendelea na mazoezi leo ikiwa ni siku ya tatu mfululizo.


Yanga imekuwa timu iliyoanza mazoezi mapema ikilinganishwa na timu nyingine za Dar es Salaam.
 
Kocha Hans van der Pluijm amesema wataendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Karume, Ilala.

"Ukianza mapema, unakuwa na nafasi ya kuamua mambo mengi, ubadili nini au uongeze kipi. Kuanza mapema pia kunasaidia wachezaji kuwa fiti zaidi," alisema.


Hata hivyo Yanga imekuwa ikifanya mazoezi na baadhi tu ya wachezaji wake kwa kuwa wengine wako katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, pia Rwanda.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic