June 24, 2015


Kocha Mkuu wa Yanga Mholanzi, Hans Pluijm ametamka kuwa wachezaji wawili wa Ghana wakati wowote wanatarajiwa kutua nchini kujiunga na kikosi hicho kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika, mwakani.


Kauli hiyo, ameitoa ikiwa ni siku chache tangu Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia kamati yao ya utendaji kuruhusu klabu za ligi kuu kusajili wachezaji saba wa kimataifa.

Waghana hao, walitakiwa kuwepo kwenye msafara wa kocha huyo akitokea Ghana kwenye mapumziko, lakini sheria za wachezaji watano zikawazuia nyota hao kutua nchini kujiunga na Yanga.
Pluijm hana taarifa ya idadi ya wachezaji wa kimataifa kuongezwa kwenye timu shiriki za ligi kuu, hivyo mara atakapopewa taarifa za kiofisi na viongozi haraka nyota hao watatua.

Pluijm alisema, hawezi kutaja nafasi za wachezaji hao watakaotua kuichezea Yanga, hivyo  mashabiki wasubirie kuwaona wakiwa uwanjani.

 “Mimi sina taarifa ya idadi ya wachezaji kuongezwa kufikia saba, mimi nasubiria taarifa rasmi kutoka kwa viongozi wangu na kama ni hivyo basi tutaongeza wengine wawili wenye uwezo mkubwa tutakaowatumia kwenye michuano ya kimataifa.

“Wapo wachezaji wawili raia wa Ghana niliotakiwa kuongozana nao hapa nchini tayari kwa kujiunga na Yanga, lakini ikashindikana kutokana na TFF kugoma kuongeza idadi ya wachezaji wa kimataifa.
“Hivyo, kama TFF wameruhusu kuongeza idadi ya wachezaji na kufikia saba, basi hao Waghana watakuja kujiunga na Yanga na hadi sasa wapo tayari ,”alisema Pluijm.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic