Viungo washambuliaji wapya wa Yanga, Deus
Kaseke na Geofrey Mwashiuya taratibu wameanza kuingia kwenye kikosi cha kwanza
Mholanzi, Hans Pluijm, atakachokitumia kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na
Ligi ya Mabingwa Afrika.
Wachezaji hao wote wanacheza viungo
washambuliaji wanaotokea pembeni kwa upande wa Kaseke yeye anacheza namba 7
inayochezwa na Simon huku Mwishiuya akicheza 11 ambayo kwenye msimu uliopita
ilikuwa ikichezwa na Andrey Coutinho.
Kaseke amejiunga Yanga hivi karibuni
akisaini mkataba wa miaka miwili akitokea Mbeya City huku Geofrey Mwashiuya
aliyetokea Kimondo FC iliyokuwa
inashiriki Ligi Daraja la Kwanza.
Katika mazoezi ya jana asubuhi yaliyofanyika
kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, Pluijm alionekana akiwapa mbinu
mbalimbali za ndani ya uwanja viungo hao.
Kocha huyo, aliwapa mbinu za jinsi ya kupiga
krosi kwa washambuliaji kabla ya kufunga mabao wakati timu inashambulia goli la
timu pinzani.
Wakiendelea na mazoezi hayo, kocha huyo
alisikika akiwataka viungo hao kuinua macho na kuwaangalia washambuliaji wao
kabla ya kupiga krosi hizo ili mpira umfikie mchezaji mwenzake.
Viungo hao, pia wakati mwingine walitakiwa
kufunga wenyewe mabao pale wanapopata nafasi ya kupiga mashuti ndani au nje ya
18 ya uwanja.
Akizungumzia mbinu hizo, kocha huyo alisema
kuwa :“Mazoezi ya stamina, nguvu na pumzi tayari nimemaliza na nilichobakisha
hivi sasa ni mazoezi ya mbinu ya jinsi ya kufunga na kuzuia mabao golini kwetu.
“Mazoezi hayo ya mbinu nitaendelea nayo kwa
kipindi kirefu, kama unavyoona tumesajili wachezaji wapya ambao bado hawajaujua
mfumo ninaoutumia, hivyo natumia muda huu kuwapa mbinu nitakazozitumia,”alisema
Pluijm.
Aidha katika hatua nyingine, Pluijm alisema
kuwa upo uwezekano mkubwa wa kikosi chake kwenye msimu ujao wa ligi kuu kuwepo
na mabadiliko baada ya kusajili wachezaji wapya.
Mbali na hawa wachezaji wengine ambao
walikuwa na kina Kaseke ni Kpah Sherman, Salum Telela, Malimi Busungu na Juma Abdul.
0 COMMENTS:
Post a Comment