SINGANO 'MESSI' KULIA AKIWASILI KATIKA MAKAO MAKUU YA TFF AKIONGOZANA NA MWENYEKITI WA SPUTANZA, MUSSA KISOKO (KUSHOTO). |
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza kwamba
klabu ya Simba na kiungo Ramadhani Singano ‘Messi’ watakaa na kujadili mkataba
wao upya.
Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine amesema
wamegundua mikataba miwili alionao Messi na walionao Simba, ina matatizo.
“Hivyo tumekubaliana waanze mwanzo kujadili tena
ingawa ni muhimu kuzingatia mkataba mama,” alisema Mwesigwa.
Suala la kuzingatia mkataba mama ambao ndiyo ule wa
Simba, nalo limeonekana kuzua utata jambo ambalo limezidi kuwachanganya hata
waandishi lakini katibu huyo alipoulizwa, alijibu.
“Hatujaja hapa kutangaza mshindi ni nani, kwa kifupi
ni vizuri waanze upya na kujadili kuhusiana na mkataba mpya,” alisema.
Messi alikuwa na mkataba unaoiisha 2015, wakati Simba
wana mkataba unaoisha 2016 jambo lililozua tafrani kati yao.
Licha ya Mwesigwa kukiri kulikuwa na mapungufu pande
zote mbili baada ya kikao hicho cha pande zote pamoja na Sputanza, bado
alishindwa kuweka wazi kama Messi bado ni mchezaji wa Simba au makubaliano
yanamfanye awe huru.
“Siwezi kuweka hadharani masuala yanayohusu mkataba,
hiyo ni siri kati ya mchezaji na klabu,” alisisitiza.
Wajumbe wa kikao cha leo walikuwa ni hawa:-
- Collin Frisch - Simba
SC
- Ramadhan Singano
- Mchezaji
- Mussa M. Kissoky
- SPUTANZA
- Mwesigwa J. Selestine
- Katibu Mkuu - TFF
0 COMMENTS:
Post a Comment