MKUTANO WA USULUHISHI KATI YA SIMBA NA MESSI, UKIENDELEA HUKU KUKIWA NA WAWAKILISHI WA TFF NA SPUTANZA. |
Kiungo Kiungo Ramadhani Singano ‘Messi’ amesema kwa
mujibu wa majadiliano kati yake na klabu ya Simba, sasa ni mchezaji huru.
Messi amesema hayo leo mchana mara baada ya mkutano
kati yake na Simba uliosimamiwa na TFF na kuhudhuriwa na Chama cha Wanasoka (Sputanza).
Kikao hicho cha usuluhishi kilifanyika leo katika
ofisi za TFF na Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine amesema wamegundua
mikataba miwili alionao Messi na walionao Simba, ina matatizo.
Lakini Messi alisema hakuwa akielewa vizuri suala la
kwamba wakubaliane katika mkataba mpya.
“Kwa mujibu wa mazungumzo ni kwamba mikataba yote
miwili imefutwa. Sasa tunatakiwa kujadili mkataba mpya, kama ni hivyo mimi ni
mchezaji huru.
“Pia sielewi kuhusiana na suala la pili, mfano
tukishindwana na Simba, itakuwaje,” alihoji Messi.
Suala hilo linaonekana kwisha, lakini kumekuwa na
utata na Mwesigwa alionekana kushindwa kulifafanya vizuri kama mkataba wa
unaoishia mwaka 2015 au ule ulioelezwa kuishiwa mwaka 2016 ndiyo ulikuwa
sahihi.
Wanahabari walitaka kujua tatizo lililokuwa kwenye
mkataba lilikuwa ni lipi hasa. Lakini bado kulionekana kuwa na ugumu kwa watoa
ufafanuzi akiwemo Mwenyekiti wa Sputanza, Mussa Kisoki.
Kushindwa kuelezewa vizuri kwa suala hilo kutoka TFF
na Sputanza, pia Messi kuonekana haelewi vizuri kilichotokea, ilisababisha maswali
mengi.
Hata hivyo, Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Simba, Haji
Manara amesema kamati ya utendaji ya klabu huyo inakutana kesho na mwisho
itatoa tamko kuhusiana na suala hilo.
Simba imekuwa ikisisitiza kuwa ina mkataba na Messi wa
miaka mitatu unaoisha mwaka 2016 lakini yeye anasisitiza alikuwa na mkataba wa
miaka miwili na klabu hiyo na unaisha Julai mwaka huu.
Hapo mzee mzima aliboronga, kwahiyo wanajaribu kumfichia aibu!! Si mara ya kwanza kwa hawa jamaa kucheza na mikataba ya watu!!
ReplyDeleteSimba wamejaa watu waujanjaujanja yaani makanjanja sana tuu.Yule baba mwenye kipara alihusishwa kumpindua baba wa taifa,rais wao ni tapeli namba moja dar,makamu ni msanii ile mbaya mwenyewe anajiita mtoto wa mjini,mjumbe mwingine ndiye masterplan wa kughushi sahihi za wachezaji na hata msemaji wao alihusishwa na wizi wa magari na utapeli.
DeleteHivyo kamati nzima ya utendaji ni watu waujanjaujanja tuu hakuna maendeleo ya klabu ila mifuko yao tuu.