June 25, 2015


Kikosi cha timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U-15) kesho Ijumaa kinatarajia kusafiri kwenda jijini Mbeya kwa ajili ya mchezo wa kirafiki na timu kombani ya mbeya U15.


U15 ambayo inanolewa na kocha Bakari Shime, itaondoka na kikosi cha wachezaji wa thelathini (30) ambapo wanatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki na timu ya kombani ya mkoa wa Mbeya ya vijana wenye umri chini ya miaka 15.

Timu itacheza michezo ya kirafiki siku ya jumapili na jumatatu ambapo kocha Shime atatumia nafasi hiyo kutambua uwezo wa wachezaji wake na kuongeza wachezaji wengine watakaonekana kutoka katika kombani ya mkoa wa Mbeya.

Mwezi ujao kikosi cha U-15 kitaelekea kisiwani Zanzibar kucheza michezo ya kirafiki na timu za kombaini ya Zanzibar kisha baadae kuendelea na ziara ya kucheza michezo ya kirafiki katika mikoa ya Iringa, Morogoro, Tanga, Arusha, Mwanza na Dodoma.

Lengo la TFF ni kuhakikisha Tanzania inakua na kikosi bora cha timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 kitachoshiriki kuwania kufuzu kwa fainali za vijana Afrika wenye umri chini ya miaka 17 mwaka 2017 nchini Madagascar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic