BOSI WA BIN SLUM TYRES, NASSOR BIN SLUM, NASSOR BIN SLUM (KULIA) SIKU ALIPOINGIA MKATABA NA NDANDA FC. |
Na Saleh Ally
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), leo limefanya jambo zuri ambalo
linapaswa kupongezwa.
Imefanyika hafla fupi ambayo iliambatana na uzinduzi wa jezi mpya lakini
pia kuwatuza watu mbalimbali kwa mchango wao.
Mchango wao ulitambulika hivi, kwamba ni watu walioshiriki katika
maendeleo ya mpira wa miguu katika kipindi cha miaka 50 tokea Tanzania
ilipojiunga na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Kuwakumbuka waliotoa mchango ni jambo jema. Niliona baadhi ya waandhishi
pia wakituzwa, ingawa wako kadhaa walisahauliwa kama Salva Rweymamu ambaye sasa
ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu.
BIN SLUM AKIINGIA MKATABA NA STAND UNITED. |
Huku ni kati ya waandishi wa mwanzo kabisa wa gazeti la Dimba ambalo ni
la kwanza la michezo nchini. Nilifundishwa kazi pale na mmoja wa walimuwa wangu
alikuwa ni Rweymamu akiwa na wengine kam Jenarali Ulimwengu ambaye alituzwa.
Kusahaulika inatokea, lakini niliona ni vema kuzungumzia kuhusiana na
wadhamini baada ya kuona wengi wametuzwa.
Listi ya wadhamini waliotuzwa ni hii hapa;
WADHAMINI
113. TBL
114. VODACOM
115. SERENGETI BREWERIES
116. NMB
117. AZAM
118. BAHATI NASIBU YA TAIFA
119. AIRTEL
120. BANK ABC
121. COCA COLA
122. NSSF
123. AZAM MEDIA
124. BARRICK GOLD MINE
125. AIR TANZANIA
126. TANZANIA RAILWAY CORPORATION
127. SYMBION
128. TANZANIA TOBACCO BOARD
129. TANZANIA COFFEE BOARD
130. TANZANIA SISAL BOARD
131. TANZANIA HARBOUR AUTHORITY
132. BIMA
133. UHAMIAJI
134. BORA
135. URAFIKI
136. TACOSHILL
Walichofanya ni vizuri, lakini TFF lazima ikubali
kwamba inaendeleza mpira kwa kushirikiana na klabu za soka amabzo ndiyo
zinabeba mzigo mkubwa.
Hata wachezaji wanaokwenda katika timu ya taifa
wanatokea katika klabu. Hivyo klabu ni uti wa mgongo wa mwili wa TFF.
Moja ya wadhamini ambao kwa moyo wa dhati naweza
kusema walipaswa kupongezwa ni kampuni ya matairi ya Bin Slum Tyres ya jijini
Dar es Salaam.
Huenda hata kungekuwa na tuzo maalum kwa kampuni kwa
sababu mbili tu. Kwanza inaingia ndani ya hiyo miaka 50 ya Tanzania kujiunga Fifa.
Pili imekuwa ni kampuni, licha ya kufanya biashara
lakini wahusika wameonekana wanapenda mpira kwa dhati huenda hata kuliko
kuangalia watapata nini.
Kwa timu hizo tatu walimwaga zaidi ya Sh milioni 500. Hiki
si kitu kidogo kutoa fedha kama hizo kwa timu kama Mbeya City, Ndanda FC na
Stand United.
Mbeya City ilikuwa ndiyo ina msimu wa pili, Ndanda na
Stand ndiyo zilikuwa zimepanda daraja. Lakini kampuni hiyo haikujali.
Tunajua kila timu inayokwenda kudhamini soka, lazima
inaangalia kwanza Yanga na Simba na ingekuwa tayari kufanya hivyo hata kama
jina la kampuni yake litawekwa mgongoni.
Nani aliuona ujasiri huo wa Bin Slum ambao umekuwa
changamoto kwa timu hizo tatu kuhakikisha zinabaki Ligi Kuu Bara.
TFF lazima ikubali, waliofanya kazi na TFF direct na
indirect wote walistahili kutuzwa. Mtu kama Bin Slum anachangia kuipunguzia TFF
presha kwa kuwa timu zinapokuwa na udhamini, kuna mambo mengi yanajitokeza.
Uhakika wa safari, kuwalipa wachezaji makocha na
viongozi, lakini inasaidia kuongeza ushindani katika ligi ambayo ni mali ya TFF
na dada yake Bodi ya Ligi.
Inawezekana kweli walisahau, lakini msisitizo, siku
nyingine bora kuwaangalia watu wenye mapenzi ya dhati kama kampuni ya Bin Slum,
angalau kuwaambia ahsante, ingekuwa ni dawa tosha ya kuona kumbe na mpira nao
unawajali, basi wangeendeleza undugu wa dhati.
0 COMMENTS:
Post a Comment