Kocha wa Yanga, Hans van
der Pluijm amewaeleza memba wake wa benchi la ufundi kwa msimu huu hakutakuwa
na mzaha hata kidogo.
Pluijm raia wa Uholanzi
amewataka kufanya kazi kwa juhudi kwa kiwango cha juu ili wahakikishe wanafanya
vizuri nyumbani Bara lakini nguvu nyingi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa
Afrika.
“Kweli kocha kasisitiza
sana kwamba msimu ujao ni kazikazi. Hakutakuwa na nafasi ya utani hata kidogo.
“Ameanza na watu wa
benchi la ufundi na baadaye atashuka hadi kwa wachezaji. Kweli anataka tufanya
kazi vizuri na kufanya vizuri hapa nyumbani.
“Lakini amesisitiza sana
kuhusiana na Ligi ya Mabingwa Afrika na kasema hicho ndiyo kipimo sahihi,”
kilieleza chanzo cha uhakika.
Msimu uliopita, Yanga
ilionyesha kiwango cha juu kabisa na kuweza kufanikiwa kutwaa ubingwa ikiwa na
mechi mkononi.







0 COMMENTS:
Post a Comment