Umeona namna JKT ilivyopania
kujiimarisha zaidi katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
Makamu Mwenyekiti wake, Meja Hassan
Mabena ameonyesha wazi hawataki mchezo baada ya kumnasa mshambuliaji wa Mbeya
City, Saad Kipanga.
JKT imemnasa Kipanga na hivi karibuni
alisaini mkataba wa miaka miwili kuichezea JKT.
MejaMabena kwa kushirikiana na katibu
wa JKT, Ramadhani Madoweka wamekuwa wakiendesha zoezi la usajili.
Wamesema lengo ni kujiimarisha kwa
ajili ya msimu ujao na hawajaishia hapo, wanaendelea kusajili vifaa zaidi.








0 COMMENTS:
Post a Comment