July 31, 2015


Fainali ya Kombe la Kagame sasa itakuwa ni Azam FC dhidi ya Gor Mahia ya Kenya kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumapili.


Azam FC imekuwa ya pili kuingia fainali kwa kuitwanga KCCA kwa bao 1-0 huku Gor Mahia ikiwa imetangulia baada ya ushindi dhidi ya timu ngumu ya Al Khartoum.

Hii ni mara ya pili kwa Azam FC kuingia fainali ya Kagame, mara ya kwanza ikiwa ni 2012 ambapo ilifungwa na Yanga iliyokuwa ikifundishwa na Tom Saintfiet ambaye sasa ni kocha wa timu ya taifa ya Togo.

Mechi ya fainali itachezwa Jumapili, ikitanguliwa na ile ya mshindi wa tatu kati ya KCCA dhidi ya Al Khartoum.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic