SIMBWA |
Kocha Mkuu wa KCCA, Sam Simbwa amesema haikuwa siku yao kwa kuwa bahati ilikuwa kwa Azam FC.
Simba raia wa Uganda amesema kikosi chake kimefungwa bao 1-0 dhidi ya Azam FC iliyotinga fainali ya Kombe la Kagame kwa kuwa walikuwa na bahati.
"Tulistahili kushinda, lakini haikuwa siku yetu, Azam walikuwa na bahati ndiyo maana wameshinda.
"Nawapongeza na kuwatakia kila la kheri katika fainali, siku moja tutakutana tena na kushindana tukitaka kushinda.
"Mpira wakati mwingine unatakiwa kukubali mambo yanayotokea, hauwezi kuzuia kila kitu," alisema Simbwa.
Azam FC imeshinda bao 1-0 dhidi ya KCCA na kutinga fainali ya Kagame, huko itakutana na Gor Mahia mechi itakayopigwa Jumapili.
0 COMMENTS:
Post a Comment