Ndoto
za Yanga kutinga nusu fainali ya michuano ya Kagame na kutwaa ubingwa wa Kombe
la Kagame kwa mara ya sita, zimeishia njiani.
Waliofanya
kazi hiyo ya kuzima ndoto za Yanga kutaka kuifikia Simba iliyobeba mataji sita,
ni Azam FC.
Azam
FC imeng’oa Yanga kwa kuitwanga kwa mabao 5-4 yote yakiwa ni ya miwaju ya penalty.
Katika
mechi hiyo kwenye Uwanjawa Taifa jijini Dar es Salaam, timu hizo zilimaliza
dakika 90 kwa sare ya 0-0.
Kombe linaenda Kenya,au Sudan.
ReplyDelete