Kocha
wa zamani wa Simba, Zdravko Logarusic bado mambo yake hayakajaa vizuri nchini
Kenya.
Kwani
matumaini ya Leopards kuchukua ubingwa yanaonekana ni madogo baada ya kuchapwa
mabao 2-1 na Sony Sugar ikiwa ugenini.
Kipigo
hicho kimeifanya timu hiyo ya Logarusic kubaki katika nafasi ya 5 ikiwa na
pointi 34 baada ya mechi 20.
Inaonekana
haitakuwa lahisi kuishika Gor Mahia timu aliyoifundisha zamani kwa kuwa sasa
iko kileleni pamoja na Tusker ambayo inaonekana kuchangamka wakati Gor
ikipambana kwenye Kagame jijini Dar es Salaam.
0 COMMENTS:
Post a Comment