KATIKA PITAPITA, TUMEPATA BARUA YA MWENYEKITI WA YANGA KUPITIA MTANDAO WA www.manjivsmengi.com IKIELEZA MAMBO MENGI NA MWALIKO WA MDAHALO AMBAO MANJI AMEUTOA KWA MENGI.
MDAHALO HUO UNAFANYIKA IJUMAA HII NA UTARUSHWA MOJA KWA MOJA NA TBC KUANZIA SAA 12 JIONI HADI SAA 1 USIKU. SOMA BARUA HIYO.
Hisia
za Bwana Mengi kwenye vyombo vya habari kuwa kampuni yangu inamiliki fedha za
serikali chini ya Commodity Import Support (CIS)
Mengi
ametupa lawama akizishutumu kampuni kama Farm Equip, Apollo Tires, Quality
Garage (sasa inaitwa QG Engineering) kuhusika na ufisadi huo wa Sh bilioni
9.055.
YANGA
ilikuwa chombo muhimu wakati wa utafutwaji wa uhuru wa nchini yetu ya
Tanganyika na baadaye Tanzania. Vikao vya Chama cha TANU ilifanyika katika
makao makuu ya klabu hii kongwe.
Vikao
vilivyosaidia kuwaondoa wakoloni na kupatikana kwa uhuru wa Tanganyika.
YANGA
ilikuwa ni chombo muhimu katika muungano wa Tanganyika na Zanzibar na ndiyo
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tuliyonayo sasa.
Rangi
tatu za Yanga ziko katika bendera ya Tanzania, sehemu ya jina lake iko katika
wimbo wa taifa, mwenge wa uhuru ni sehemu ya utambulisho wa klabu hii.
Mwananchama
namba moja wa klabu ya YANGA ni hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere. Marehemu Mzee Karume ndiye aliyejenga makao makuu ya klabu ya YANGA
ikiwa ni sehemu ya shukurani wake katika klabu kwa kutoa mchango mkubwa katika
mapinduzi ya Zanzibar.
YANGA
haimilikiwi na mtu mmoja, ni ya wanachama pamoja na Wajumbe wa Bodi ya
Wadhamini inayowajumuisha Mama wa Taifa, Mama Fatma Karume. Wengine ni
Mheshimiwa George Mkuchika ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora,
mmoja wa watu wanaoheshimika katika taifa letu.
Si
viongozi pekee ambao ni mashabiki wa Yanga, hata watu wa nchi jirani pia
walipoishi hapa nchini kwa ajili ya kupambana kupata uhuru wa nchini zao
walijikuta kwenye mapenzi makubwa na Watanzania kutokana na ukarimu wao. Kama
walivutiwa na Watanzania ambao wengi ni mashabiki wa Yanga, hili halina ubishi
na kwa kuwa mimi ni Mwenyekiti wa Yanga, nawatakia kila la kheri popote walipo.
Mimi
ni Yusuf Mehbub Manji (39), Mwenyekiti kijana zaidi kutoka katika klabu ya
Yanga.
Nilichaguliwa
Julai 14, 2012 kwa ushindi wa 97.5%. Inapofikia hatua mwenyekiti wa klabu kubwa
na kongwe kama YANGA kuitwa ni mwizi, fisadi na mla rushwa na kadhalika
inanifanya nifikie uamuzi wa aina mbili.
Moja
ni kuachia ngazi au nichukue uamuzi wa pili wa kujibu kwa Wanayanga, Watanzania
na Afrika nzima. Kwani kukaa kimya ni kuleta maumivu na dharau kubwa kwa klabu
hii kongwe na watu wake ambayo kazi yake kubwa ni kuwapa furaha Wanayanga na
wapenda michezo.
Katika
taarifa iliyoandikwa katika gazeti la NIPASHE la Juni 8, 2015 lililo chini ya IPP
Media, inayomilikiwa na Bw. Reginald Abraham Mengi, inaeleza kuwa Kampuni zangu
(limezitaja Farm Equip Tanzania and Quality Garage <sasa inaitwa QG
Engineering>) zimefanya ufisadi kwa serikali ya Tanzania unaofikia Sh
bilioni 9.055 chini ya Commodity Import Support.
Taarifa
hiyo ilitoka katika vyombo vya habari vya Bw. Mengi pekee. Ukweli ni kwamba
habari hizo ni uongo mtupu, tena wa kupindukia kuhusiana name unaonezwa na
vyombo hivyo vya habari vya Bw Mengi.
Mwenyekiti
wa YANGA si fisadi, mwizi, mungo kama ambavyo taarifa zinazosambazwa na vyombo
hivyo vya habari vya adui namba moja wa klabu ya Yanga Reginald Abraham Mengi.
Mwenyekiti
huyu wa YANGA kamwe hapokei mshahara wala posho yoyote kutoka klabu. Hapati
faida yoyote ya kifedha zaidi ya kuwa zawadi ya aina yake na kipekee kwa
wengine na kuwa mtu anayeweza kuwapa furaha wengine.
Zawadi
hiyo aliyonayo mwenyekiti wa YANGA ni furaha ya wengi hasa pale timu inapofanya
vizuri kwa kushinda mechi zake na makombe na kuwapa mamilioni furaha ya moyo na
kuwafanya wasahau matatizo yao na ndiyo furaha na malipo yangu.
Kwa
wale ambao wanaweza kumkumbuka Mengi, alijaribu kutaka kuingoza Yanga katika
miaka ya 1990 lakini wazee walimfukuza. Hii ilikuwa ni baada ya kugundua
alikuwa akichochea migogoro ili aweze kuingoza Yanga kwa maslahi yake binafsi.
Wakati
wa mkutano wa wanachama uliofanyika katika Hoteli ya Starlight na Bw Mengi
kulazimika kujificha chooni baada ya walinzi wake binafsi kuzidiwa na hasira za
wanachama. Nakumbuka mwanachama mmoja alimueleza hivi: …” ungeenda kwanza
kumaliza matatizo ya ndoa yako kuliko kuendeleza mgogoro katika klabu yetu
(kweli mgogoro ambao aliutengeneza kwa makusudi).” Baada ya siku hiyo
kufanikiwa kuokolewa na Polisi, hakuwahi tena kurejea Yanga.
Mwanzoni
mwa 2006, wakati ndiyo nikiwa na umri wa miaka 36, niliombwa kuingia kuisaidia
klabu ambayo ilikuwa katika hali mbaya kifedha. Kwamba niwe mdhamini mkuu na siku
chache baadaye taarifa zilimfikia Bw Mengi ambaye alionekana kutofurahia na
Machi 26 alianza kutumia magazeti yake kunishambulia kwa nia ya kunichafua
kwamba mimi ni mhalifu, muongo na fisadi.
Kwa
kuwa nilikuwa ni mwananchi wa kawaida, si kiongozi wa klabu kubwa kama Yanga,
niliamua kutafuta haki yangu kwa kumfungulia kesi mahakamani. Kesi ambayo
nilishinda na yeye kutakiwa kunilipa Shilingi 1.
Nilipohoji
uwezo wa kufikiri, kutafakari na kuamua wa mengi, aliamua kunifungulia kesi
akidai nimlipe Sh bilioni 150, mwisho alishindwa na sasa anatakiwa kulipa kiasi
cha Sh bilioni 5 kwa uendeshaji wa kesi.
Nawakumbusha
kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita Bw Mengi alifungua kesi kesi mbili, moja
akipoteza na nyingine alimua kujitoa au kuifuta mwenyewe. Hii inaonyesha kiasi
gani kumekuwa na ukweli katika yale ambayo nimekuwa nikimueleza.
Kabla
sijachaguliwa kuwa mwenyekiti wa YANGA mlinijua, mlijua nilikuwa mtu
ninayekipigania ninachokiamini na kama nilikiamini kitu, basi ilikuwa ni njia
yangu sahihi ya kushinda.
Najua
kwa wanachama wa Yanga wamekuwa wakiona namna Mengi anavyonishambulia katika
vyombo vyake vya habari lakini wamekuwa wakipuuzia na kunipa heshima yangu kama
mtu niliomaliza mgogoro mkubwa na mgawanyiko ndani ya klabu ya Yanga ambao
niliumaliza ndani ya miezi mitatu tu baada ya kuwa mdhamini mkuu wa klabu.
Niliunda
bodi ya kwanza ya wadhamini kwa kuwaomba wazee waanzishe baraza lao. Halafu
mimi nilijiuzulu kwa kuwa nilikua ni kijana mno, miaka 33 nisingefaa kuwa mmoja
wa wajumbe wa baraza la wadhamini. Mwisho nikaaga kwa kuwa kazi yangu ilikuwa
imekwisha.
Wazee
wa Yanga waliamua kufanya dua maalum kwa ajili yangu, wakanisimika na kunifanya
kuwa CHIFU wa kwanza wa klabu kwa kunipa ngao yenye nembo ya klabu pamoja na
mkuki.
Nilipotakiwa
kwa mara nyingine katika klabu, nikiwa na miaka 36 nilichaguliwa kuwa
Mwenyekiti wa klabu kongwe ya YANGA.Kitu ambacho najivunia kwa kuwa kiongozi
kwani hata familia yangu imekuwa ikipata heshima kutoka kwa wanachama na
mashabiki wa Yanga.
Wakati
mwingine mama yangu anapokwenda sokoni, wakati mwingine hatakiwi hata kulipa
kutokana na heshima ya kuwa mama wa Mwenyekiti wa Klabu yenye heshima ya YANGA. Mmenipa heshima kubwa, mfano watoto
wangu katika akaunti zao za Facebook hawawezi hata kuweka picha yangu kwa hofu
ya kupata marafiki wengi kupindukia.
Mke
wangi analazimika hata kutumia jina tofauti kwa kuwa mapenzi makubwa anayopata
kutoka kwa mashabiki wa klabu ya YANGA yanafikia hadi kumpa hofu na hii ni kwa
kuwa wanachama na mashabiki wanajua huyu ni mke wa mwenyekiti wao ambaye
wanamuamini na kumpenda sana.
Kwa
mapenzi haya ninayopata ninaahidi nitaendelea kufanya kila ninaloweza kwa uwezo
wangu wa juu, hali na mali kwa klabu katika kipindi changu chote wakati nikiwa
mwenyekiti. Mapambano yanaendelea kwa ajili ya klabu yetu.
Tokea
Bw Mengi alipofukuzwa na wanachama wa YANGA, amekuwa mwoga kuhusiana na maisha
yake, amejaa hofu akidhani kuwa kila Mtanzania anataka kumuua! Anaomba ulinzi
wa Jeshi la Polisi huku akiwa hajui asilimia kubwa ya askari Polisi nao ni
YANGA.
Nashangaa
alitaka Yanga iharibikiwe kabisa, lakini yeye ndiye anayekimbilia katika
runinga akidai kuna watu wanatanga kumuua. Bw Mengi, YANGA haitaki kukuua,
lakini tunakuchukia ingawa tumekuwa wastaarabu na tunajizuia. YANGA tunachotaka
ni wewe kutuacha tuendelee na maisha yetu na familia yetu, endelea na yako.
Tungependa
hata usizungumzie jina la klabu yetu kupitia kalamu yako wala midomo yako.
Lakini
inaonekana kama shetani, umekuwa ukijaribu kurejea katika klabu ya YANGA tena
ukionyesha umepania kutufelisha kitu ambacho kamwe hauwezi kufanikiwa hata
kidogo. Hauwezi ukashinda uimara wa
mioyo yetu ambayo imeunganika na kuwa kitu kimoja. Unaonekana unataka kutumia
nafasi hii kurejea na kuomba msamaha kwa mabaya ulioifanyia klabu.
Kama
kweli sisi Watanzania tunajulikana dunia nzima kama ni watu tunaoishi kwa
amani, watu wenye upendo na wakarimu kwa nini kila mwaka unalalamika kuwa kuna
watu wanataka kukua? Au ndiyo ndoto mbaya zinakuandama kutokana na mabaya
uliyoyafanya huko nyuma, hivyo unataka kuomba msamaha?
Bw
Mengi, mimi sihitaji kulilia ulinzi kama unaotaka wewe. Ulinzi wangu ni
mamilioni ya Wanayanga waliopo. Sihitaji fedha ninapotembea sehemu yoyote ya
Tanzania kwa kuwa hakuna Mwanayanga anayehitaji fedha kutoka kwangu.
Sihitaji
tuzo yoyote ili nijulikane au matangazo ili wanijue, hakuna Mtanzania
asiyenijua. Pia sihitaji pasi ya kusafiria ya kibalozi ninapokuwa uwanja wa
ndege. Kama ni heshima ya red carpet, basi ninaipata kwa kuwa Mwenyekiti wa
Yanga ambaye ni mkweli na muwazi.
Ntaendelea
kuwa mwenyekiti mwaminifu ninayejitolea kwa uwezo wangu wote kwa klabu
ninayoingoza, kama siku itafikia kifo. Basi nitakuwa na uhakika watoto na
familia yangu itakuwa katika mikono salama ya wanachama na mashabiki wa YANGA
ambao wamesambaa dunia nzima.
Bw
Mengi, mimi ni mtu wa kawaida tu niliyelelewa na baba ambaye wakati wa vita ya
kumng’oa Nduli Iddi Amini Dada alitengeneza bodi ya gari maalum kwa ajili ya
wanajeshi wa Tanzania waliokwenda kupambana ambao baadaye walimshukuru kwa
kutembelea sehemu aliyokuwa akitumia kutengenezea mabodi hayo.
Tokea
hapo, kila Rais alitembelea katika gereji yake hiyo ndogo. Nilifunga ndoa mwaka
1994, ilihudhuriwa na wageni kama Mheshimiwa Rais Ali Hassan Mwinyi, Marehemu
aliyekuwa Wazidi Mkuu, Cleopa Msuya, Mheshimiwa John Malachela na viongozi
wengi wakubwa. Sasa nina watoto wawili wa kiume, mmoja akiwa na umri wa miaka
17 na mwingine 12.
Nakuuliza,
ulikuwa wapi wakati wa vita vya Kagera pia ndoa yako ya sasa ina umri gani?
Haujawahi
kuchaguliwa hata kuwa myampara tu wa gereza, lakini ajabu unajidanganya
mwenyewe eti ni kiongozi bora.
Tunajua
haukufurahia Yanga kushinda taji lake la 25 la Ligi Kuu Bara msimu uliopita! Kumbuka
Mataji 50 tu ymegombewa, hivyo Yanga imebeba nusu ya hayo hadi sasa. Haufurahii
kuona kijana mdogo kama mimi napendwa na watu wengi kuliko wewe, ndiyo maana
umekuwa ukiamua kujipamba kama vile vitabu vya ujanjaujanja kwamba wewe ni kati
ya watu matajiri zaidi Tannzania!
Mtu
usiye na huruma kuamua kupitia viwanda vyako kuchanganya dawa kutoka Marekani
na maji ya Tanzania na kuyaita Coca-Cola, kuchanganya kalamu na karatasi na
kuita taarifa! Kujionyesha wewe mwenyewe kwenye runinga yako, halafu unataka
watu waamini hiyo ni taarifa kwao!
Unawalazimisha
wanasiasa wakuombe ardhi au migodi ili uiendeleze wakati hauna mtaji wa kufanya
hivyo! Waliogundua kuwa huna uwezo huo unawashambulia kwa madai wamewapa wageni
na ungepewa wewe migodi ya gesi ungeweza kutuwasaidia sisi Watanzania masikini.
Kama
sikosei thamani yako ni dola milioni 550, unapata faida ya 10%. Mfano dola
milioni 55 utatakiwa kulipa kodi ambayo itakuwa si chini ya dola milioni 16.5
kwa mwaka. Je, umekuwa ukilipa kodi hiyo? Mimi kama Mwenyekiti wa Yanga najua
kila kitu kuhusiana na wewe.
Bw
Mengi, usitake kudanganya watu biashara uliyoanzisha miaka 10 iliyopita eti
thamani yake sasa ni dola milioni 550. IPP ilianzishwa mwaka 1981, kabla ya
hapo ulikuwa mhasibu tu. Nauliza, unafikiri YANGA hawajui kuhusiana na uhusiano
wako kwao hadi walipofikia kuniongezea muda kama mwenyekiti wao. Wanajua thamani
yangu kuliko wewe na uhasibu wako.
Ninaweza
nikakupa mfano wa biashara zangu, lengo si kujigamba. Sitaki kuzungumzia
kampuni kubwa ya uvuvi katika Ziwa Victoria au kampuni kubwa ya Rice Mill ya Morogoro.
Nitakupa mfano mmoja tu, Novemba 25, 2011 nilifungua maduka makubwa ya biashara
na mmoja wa wanasiasa wakubwa barani Afrika ambaye sasa ni Waziri Mkuu Mstaafu
wa Kenya, Mheshimiwa Railla Odinga ndiye alikuja kuyafungua akiwa mgeni rasmi
na mwalikwa siku hiyo. Wewe umefungua biashara gani kubwa ndani ya miaka 10 na
kiongozi yoyote wa Tanzania akaja kuizindua?
Maisha
yangu nimekuwa mjumbe wa bodi ya Afrika ya kupambana na ugonjwa wa ebola
maarufu kama African Union Ebola Solidarity Trust Fund ambako nimesaidia
kupatikana kwa fungu la dola milioni 50 kupambana na ugonjwa huo hatari na
kuutokomeza kabisa kwa wale ambao waliobaki wameathirika katika nchi ya Sierra
Leone.
Angalia
mashabiki na wanachama wa Yanga katika mitandao wanavyoonekana wakiwa
wameungana na wenye furaha kubwa kushangilia ushindi au ubingwa, hii
inahamasisha hata vijana. Kwa miaka 10 nimefanya makubwa kwa bara letu la
Afrika, ajabu unaona si sahihi, umeamua kufanya ujanja ujanja kwa kununua tuzo.
Najaribu kujiuliza watu wangapi watakuja katika mazishi yako kama itakavyokuwa
kwangu, kijana uliyejaribu kutaka kumharibia tokea akiwa na miaka 30, huku
ukijaribu kuniharibia biashara zangu.
Lakini
Mungu ni mwema, ameamua kunichagua kuwa mmoja wa vijana wanaopendwa zaidi
nchini Tanzania kama si Afrika kote.
Bw
Mengi, umekuwa na tabia ya kuwachafua watu kila unaposhindwa kupata unachotaka
kwamba ni wala rushwa na mafisadi! Mahakama Kuu ya Uingereza ambayo ulifungua
kesi kwa madai ya kuitwa muongo na maneno mengi, imetupa kesi yako kwa
kuonekana haikuwa na mantiki. Sasa uamuzi umekugeukia kwamba si muongozo tu au
si mwaminifu tu lakini imeonekana ni mtakatishaji wa fedha, vyombo vyako vya
habari havifuati weledi, badala yake vinafuata wewe unafuata au kufadika na
kipi!
Inaonekana
IPP hakuna uhuru wa habari na waandishi wenyewe isipokuwa kile unachotaka wewe
hadi kufananishwa na ujasusi wa habari (sawa na ule wa Osama Bin Laden wa Al-Quaeda
au ISIS kwa siku za karibu).
Kesi
hiyo imekugeukia kwamba kwa sharia za Tanzania unapaswa kushitakiwa kwa jinai
na vyombo vya sharia vya Tanzania.
Kwa
nafasi ya Mwenyekiti wa YANGA na kama mwangalizi mkuu, nitapambana kulinda jina
la klabu hii tukufu na kama Mwenyekiti wa YANGA ningependa kutangaza kumualika
Bw Mengi katika mdahalo utakaorushwa na runinga moja kwa moja Ijumaa ya Julai
3, 2015.
Watanzania
watakuwa na nafasi ya kuulizwa maswali katika mdahalo huo wa wazi na moja kwa
moja. Hii itakuwa nafasi nzuri kwa Bw Mengi kuja au kutoa ushahidi wake
kuhusiana na ufisadi wangu kwa uthibitisho. Pia utakuwa wakati mzuri kwa
Watanzania kujua nani ni mkweli na yupi hayuko sahihi.
Pia
ningependa Watanzania wapewe nafasi ta kupiga kura kwa ujumbe mfupi wa simu
(SMS) kama kweli wameona mimi ni fisadi. Kama itakuwa hivyo, basi nitajiuzulu mara
moja uenyekiti wa YANGA.
Ni
jukumu langu kama Mwenyekiti wa Yanga kumaliza upuuzi huu ambao unaozushwa na
Bw Mengi ambao unaweza kuiondoa klabu yetu katika utulivu na kuweza kufanya
mambo yake kwa mpangilio mzuri kama ambavyo tumekuwa tukitaka. Yanga imekuwa
ikiwavutia wachezaji wengi wakiwemo wa kimataifa, pia tuko katika harakati za
kuhakikisha tunajenga uwanja wetu wenyewe na YANGA yenye mipango endelevu na
thabiti.
Sioni
kama kuna sababu ya kupoteza muda wangu wa kuitumikia Yanga kwa ajili ya mtu anayewalaghai
watu kuwa yeye ni mtu mzuri, mwema, kitu ambacho ni uongo mtupu. Nasisitiza,
sasa imetosha.
Ukweli
utajulikana hiyo Julai 3, 2015 na kama Bw Mengi atakuwa na ukweli anaotaka
kuuweka wazi, basi hatasita au kukimbia kuja kukaa name mbele ya Watanzania
kwenye mdahalo. Lengo ni kumaliza ubabaishaji huu na ugaidi kupitia vyombo
vyake vya habari kwa kuwa nimechoka sasa na hali hii kwa kuwa inanichosha na
kuchukua nguvu zangu za kupambana na maendeleo ya klabu.
Klabu
ya Yanga ni tukufu katika nchi, uongo wa Bw Mengi umekuwa ukifanya hata baadhi
ya wanaotaka kufanya biashara na klabu, mashabiki au wanachama kuingoa hofu
kwamba klabu yetu inaendeshwa na fedha chafu, jambo ambalo si sahihi hata
kidogo.
Yanga
Daimba Mbele, Nyuma Mwiko. Ndiyo maana nataka huu mdahalo ili kumaliza maneno
yasiyokuwa na ukweli ya Bw Mengi kwa miaka takribani 20 sasa. Tunataka kumaliza
hilo ili tuelekeze nguvu zetu kwenye maendeleo ya klabu na kuachana na Bw Mengi
ambaye amekuwa akitumia vyombo vyake vya habari kutaka kutuvuruga kwa makusudi.
Acha
nihitimishe hili; kuwa mwisho lazima tujue ni mimi mbaya kwa Tanzania au Bw
Mengi, kiongozi huyu ambaye alitaka kura za Wanayanga lakini sasa yuko ofisini
akifanya kila analoweza kuivuruga Yanga huku akihakikisha tunashindwa katika
kila jema na bora tunalotaka kufanya kwa ajili ya klabu yetu. Waanzilishi wa
klabu yetu, taifa na viongozi tutakuwa na kila sababu ya kujilaumu wenyewe kama
tutashindwa kufikia malengo na tunachokitaka kwa ajili ya klabu yetu.
MUNGU
IBARIKI YANGA, TANZANIA NA AFRIKA.
NINAWASHUKURU
SANA.
Yusufali
Mehbub Manji
(Mwenyekiti
wa Klabu ya Yanga)
SOURCE: www.manjivsmengi.com
hao wana yao ambayo hsyahusiani na soka letu ila wameamua kutumia kivuli cha soka kuoneshana wao ni akina nani
ReplyDelete