Na Saleh Ally
TIMU
nne zimebaki katika michuano ya Kombe la Cecafa inayoendelea na Tanzania imebaki
na timu moja timu.
Wakati
michuano inaanza, Tanzania Bara ilikuwa na timu mbili ambazo ni Azam FC na
Yanga na Zanzibar ilikuwa na timu moja, KMKM.
Yanga
na KMKM wametangulia, wameng’olewa katika michuano hiyo na sasa Watanzania
wamebakiza timu moja.
Zilizobaki
zinatokea Kenya-Gor Mahia, Uganda-KCCA na Al Khartoum ya Sudan.
Kama
ni Mtanzania mzalendo, hakika atakuwa na hamu ya kuona kombe hilo linabaki
nyumbani na timu pekee inayoweza kufanya hivyo ni Azam.
Azam
ina uwezo wa kuingia fainali kwa kuwa hii si mara ya kwanza, mwaka 2010
iliingia ikiwa na Yanga, ikapoteza.
Safari
hii ndiyo timu bora kabisa ya mashindano hadi zinabaki hizo nne kwa kuwa
haijafungwa hata bao moja ndani ya dakika 90.
Maana
yake ni timu yenye uwezo wa kufanya vizuri. Kilichobaki ni kuhakikisha inaungwa
mkono kwa nguvu zote.
Jiulize
mara mbili, kama wewe kweli ni Mtanzania, unafurahi vipi kuona kombe
linachukuliwa Gor Mahia ambayo itawapelekea Wakenya au KCCA iwapelekee Waganda.
Rekodi
za michuano hiyo zinaonyesha Simba imechukua mara 6 ambayo ni nyingi zaidi.
Inafuatiwa na Yanga na Gor Mahia.
Sasa
unataka Wakenya au Wasudan waende nalo? Ili iweje? Kwa faida ya nani? Nafikiri kuna
kila sababu ya kuiunga mkono Azam FC.
Lakini
tuhakikishe inasonga hadi fainali na kubeba kombe hilo kwa kuwa hatuna uwezo wa
kuibadilisha isiwe timu ya Tanzania.
Azam
FC ni ya mwekezaji Mtanzania, hivyo hatuna uwezo wa kulibadili hilo na huu
ndiyo wakati wa kuonyesha uzalendo.
Si
lazima kwa kila mtu afanye hivyo, anayeshindwa anaweza kubaki nyumbani. Anayeona
ni muhimu kuunga mkono aende uwanjani na kuiunga mkono Azam FC kutoka Tanzania.
Sito iunga mkono azam hadi nakufa
ReplyDelete