PICHA ALIYOITUPIA MACHUPPA MTANDAO IKIMUONYESHA LOWASSA NA VIONGOZI WENGI WA JUU WA CHADEMA.
Mshambuliaji wa
zamani wa Simba, Athumani Machuppa ‘Mani’ ameonyesha wazi hisia zake kutokana
na taarifa za kuwa mwanasiasa mkongwe wa CCM, Edward Lowassa anahamia upinzani.
Machuppa anayeishi nchini Sweden ametupia picha aliyoiunganisha kutoka mtadao wa kijamii wa Twitter na kuiweka
Facebook huku akisema: “madaraka haya”.
Katika maelezo
yake, Machuppa anaonyesha kushangazwa na Lowassa kuhamia Ukawa ambao wapinzani
ndiyo waliomuita fisadi.
MACHUPPA.
Asilimia 90
wanaonekana kumuunga mkono Machuppa huku wakishangazwa na Lowassa anayeungana
na waliomuita fisadi na mwizi.
Lakini wengine
wanamuunga mkono Lowassa kwamba CCM zaidi ya miaka 50 sasa hawajaleta
maendeleo.
Mwisho Machuppa
anonyesha kuhoji, kwamba kama hakuna maendeleo, Lowassa atayaleta? Swali lake
linaonekana kuwa gumu.
Taarifa hiyo
huku picha inaonekana Lowassa akiwa na viongozi wa Chadema imezua stori nyingi
mtandaoni na watu wanajadili hasa suala la wapinzani kumtangaza Lowassa ni
fisadi na sasa wanakubali awe mgombea wao wa urais?
|
Machupa aachane na siasa acheze mpira kila mtu na fani yake... au amesahau kuwa siasa na mpira ni vitu tofauti? Kila mtu anayo hiyari ya kuhama chama kwani chama si kabila au mmesahau hata Nyerere aliwahi kusema CCM si BABA wala MAMA YAKE?
ReplyDeleteNchi hii kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni yake,nionavyo mimi Machupa ametoa yaliyo moyoni mwake kuhusiana na sakata la Lowassa kuhamia upinzani tena CHADEMA,Kwangu Mimi angehamia chama chochote cha kisiasa cha upinzani tofauti na vyama ambavyo vilimuita majina kede wa kede machafu wala nisingeshtuka,,Sasa kuhamia kule kule kwa balozi na kuanza kusafishwa hapo kwangu ndio tatizo,kwani inaonesha Chadema hawana candidate anaefaa kuwania Uraisi na kuitoa CCM madarakani?
ReplyDeleteAh ,kila mtu anaona,nionavyo hawa viongozi wetu njaa zita waua
ReplyDeleteKastaafu mpira sasa hv jamani ana haki ya kuchangia kama mtanzania lowassa nani bwana sisi tulitegemea sura mpya kumbe kuna kitu anataka mamvi pale magogoni watch out..
ReplyDelete