Kocha Mkuu wa Manchester
United, Louis van Gaal amemuonyesha kipa David de Gea kwamba akizubaa ataishia
benchi.
Van Gaal
amesema De Gea lazima aonyeshe juhudi kwa kuwa kipa wa timu ya taifa ya
Argentina aliyejiunga na Man United, Sergio Romero ana kipaji na mchapakazi.
Hata hivyo
taarifa zinasema inaonekana bado Man United ina matumaini makubwa ya kumpata
beki Sergio Ramos na De Gea aondoke kwenda kujiunga na Real Madrid wakati wa
dirisha dogo.
Kama itakuwa
hibyo, maana yake Romero atachukua namba moja. Tayari kipa huyo ameanza kujifua na kikosi cha Manchester United.
0 COMMENTS:
Post a Comment