Straika mpya wa Simba, Hamis Kiiza, amesema
atahakikisha anaitumikia ipasavyo timu yake mpya na kuipa mafanikio kama
alivyofanya wakati anaichezea Yanga.
Kiiza amejiunga na Simba hivi karibuni na
kupewa mkataba wa miaka miwili baada ya kuachwa na Yanga katika dirisha dogo la
usajili Desemba, mwaka jana.
Kiiza
amesisitiza atajitahidi kwa kadiri ya uwezo wake kuisaidia Simba ifikie malengo
yake na atacheza kwa kiwango kikubwa kama alivyofanya awali.
“Nipo Simba na nawaahidi mashabiki wasiwe na
wasiwasi juu ya kuisaidia timu hii kwenye suala zima la kupata mafanikio,”
alisema Kiiza na kuongeza:
“Nitajitahidi kuhakikisha vile nilivyofanya
nikiwa na Yanga navihamishia huku kwa sababu nimeondoka kule sikuwa na deni
hata moja kwani mataji niliwapa.”








0 COMMENTS:
Post a Comment