Kocha wa zamani wa Simba, Patrick Liewig
raia wa Ufaransa ametua nchini na rasmi kutambulishwa kuwa kocha mpya wa Stand
United.
Liewig ambaye aliifundisha Simba kwa nusu
msimu, anatarajia kusaini mkataba wa miaka mitatu kuinoa Stand United ya
Shinyanga.
Mkurugenzi wa ufundi wa Stand United, Muhimu
Kanu amesema kila kitu kimekwenda vizuri.
“Limebaki suala la kusaini mkataba tu,
litafanyika leo jioni na matarajio yetu kila kitu kitakwenda vizuri,” alisema
Kanu.
Stand ambayo imeingia mkataba wa mamilioni
ya fedha na kampuni ya uchimbaji madini ya Acasia, imepania kujiimarisha zaidi
kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
Msimu huo utakuwa wa pili kwa Stand United
iliyocheza msimu uliopita ingawa mwishoni ililazimika kufanya kazi ya ziada
kupigania ‘roho’ yake ili ibaki.








0 COMMENTS:
Post a Comment