Timu ya soka ya Jeshi la Rwanda, APR leo
Jumamosi saa 8:00 mchana inacheza mechi ya kwanza ya Kombe la Kagame dhidi ya
Al Shandy kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kikosi hicho kimedai kiungo
wake Jean Baptiste Mugiraneza ‘Migi’ amewaharibia.
Hiyo ni kauli ya Kocha Msaidizi wa APR, Vincent
Mashami wakati alipokuwa akielezea mchezo wao wa leo wa Kundi B dhidi ya Al
Shandy ya Sudan.
“Unajua Migi alikuwa mchezaji wetu tegemeo na
nahodha, sasa kuondoka kwake kumetufanya tuwe na pengo kikosini, amevuruga
mipango yetu ya kutwaa ubingwa.
“Hata hivyo, tutapambana na wachezaji tulionao
ili tuweze kufanya vizuri, kwani kumkosa Migi ni mambo ya kiuongozi zaidi ndiyo
yaliyotokea” alisema Mashami.
Migi amejiunga na Azam FC siku chache
zilizopita lakini kutokana na majeraha ya jino aliyopata katika mazoezi ya timu
hiyo, hatacheza mechi ya kesho ya Kombe la Kagame itakayoikutanisha Azam na
KCCA.







0 COMMENTS:
Post a Comment