Na Aidan Mlimila
Nakumbuka msimu uliopita siku ya
mwisho wakati dirisha la usajili la majira ya kiangazi linafungwa mwandishi
mmoja wa gazeti la Telegraph la Uingereza, Jim White aliandika "Ed
Woodward is buying everything except what's needed" akimaanisha kuwa
mtendaji mkuu wa Man Utd Ed woodward ananunua kila kitu isipokuwa kile ambacho
kinahitajika.
Jim white aliandika maneno haya kwa
sababu aliona Ed woodward ambaye ni mtendaji mkuu wa Man Utd alikuwa akisajili
wachezaji kwenye nafasi nyingine za huku zile nafasi ambazo kweli zilikuwa
zinamahitaji makubwa zikitelekezwa na hapo alikuwa akilenga nafasi ya ulinzi
sana kwenye nafasi ya ulinz wa kati na sehemu ya kiungo cha ulinzi(defensive
midfield).
Ni jambo ambalo liliweza kuonekana
dhahiri wakati ligi ilipoanza Man Utd walionekana kuwa na mapungufu kwenye
maeneo hayo although badae waliweza kukaa sawa na kumaliza ndani ya nafasi nne
za juu.
Nikijaribu kuuangalia usajili ambao
mpaka sasa ambao Man Utd wameufanya inaonekana ni kama Bw Ed woodward alimsikia
Jim White wakati alipokuwa akikosoa usajili ambao Man Utd walikuwa
wakiufanya.
Nasema hivi kwa sababu kwa usajili ambao mpaka sasa umefanyika
nikiangalia na wachezaji waliopo naiona Man Utd mpya kabisa na nina amini
itakuwa ni moja kati ya timu ambazo zitatoa changamoto kubwa sana kwenye
harakati za kuwania ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza na pengine wanaweza
kurudia kwenye zama zile za Sir Alex Ferguson.Na bado Man Utd wanaonekana
kuendelea na harakati za usajili kama ambavyo Louis Van Gaal alivyonukuliwa
akisema kuwa bado wanaendelea na usajili.
Lakini pia kitu kingine ambacho
kinanifanya niamini kuwa Manchester Utd wanaweza kurudia zama za Babu Fergie ni
namna ambavyo Louis Van Gaal amekuwa akisimamia descipline za wachezaji wake
ndani na nje ya uwanja kitu ambacho kilikuwa silaha kubwa sana ya Fergie katika
kupata mafanikio yake.
Katika timu zote ambazo Louis Van Gaal amepita kuanzia
Barca,Bayern,Timu ya Taifa ya Uholanzi(The Orange) na nyinginezo Van Gaal
amekuwa ni mtu ambaye amefanikiwa kusimamia nidhamu za wachezaji wake kitu
ambacho kimemsaidia kurahisisha kazi yake kwa kiasi kikubwa.
Van Gaal amekuwa ni mtu ambaye
hapendi mchezaji yeyote kuwa juu ya klabu isipokuwa yeye mwenyewe tabia ambazo
zinafanana na zile za Fergie kitu ambacho kwa kiasi kikubwa kilimsaidia Sir
Fergie kupata mafanikio makubwa akiwa na Man Utd ukiachilia mbali ubora wa
mbinu ambazo alikuwa akizitumia.
Ni juzi hapa tumeona Van Gaal
akimtema Victor Valdes kwa sababu aligoma kufanya mazoezi na timu ya kikosi cha
pili kinachoundwa na vijana.
Na LVG alinukuliwa akisema kwamba hawezi
kumvumilia mchezaji yeyote ambaye haeshimu na haendani na falfasa za timu na
ndiyo sababu akaamua kumtema Victor Valdes tukio ambalo nalifananisha na baadhi
ya matukio ambayo Ferguson ameshawahi kuyafanya kipindi cha nyuma kwa kuwauza
baadhi ya nyota wake ambao walishindwa kufuata kile ambacho yeye alikitaka na
kuonyesha baadhi ya matendo ya utomvu wa nidhamu wachezaji hao ni kama David
Beckham,Jaap Stam,Roy Keane,na Paul Ince.
Na hapo ndipo ambapo taratibu naanza
kuiona Manchester Utd mpya na kurudia nyakati za Sir Alex Ferguson.










0 COMMENTS:
Post a Comment