Pamoja na
kufanikiwa kucheza vizuri sana katika michuano ya Kagame, beki Serge Wawa wa
Azam FC amesema kama mchezaji hayuko fiti katika michuano ya Kagame, anaweza ‘kufa’.
Wawa alisema ‘kufa’
akimaanisha mchezaji hatafanikiwa kuendelea kwa maana ya hataweza.
Akizungumza na
SALEHJEMBE mara tu baada ya mechi yao dhidi ya KCCA ambayo wameshinda na
kutionga fainali ya michuano hiyo, Wawa raia wa Ivory Coast amesema mechi
zimekuwa zikichezwa haraka haraka kwa maana ya karibu karibu.
“Unapumzika
siku moja tu baada ya kucheza mechi ngumu kama ile dhidi ya Yanga, unarudi tena
uwanjani kucheza.
“Baada ya mechi
ngumu kama ya leo dhidi ya KCCA, tunakwenda kwenye fainali baada ya kupumzika
mechi moja tu.
“Tunakutana na
Gor Mahia, nao wako vizuri sana. Hivyo ni ushindani tena mgumu sana,” alisema
Wawa.
Wawa ameingoza safu ya ulinzi ya Azam FC kutofungwa hata bao moja hadi sasa.
0 COMMENTS:
Post a Comment