Na Saleh Ally
Robo
fainali ya Kombe la Kagame itakayopigwa Jumatano ndiyo itakuwa tamu kuliko zote
msimu huu.
Inazikutanisha
timu mbili za Tanzania, Yanga dhidi ya Azam FC.
Mechi
hiyo, hata kabla haijachezwa, tayari imezaa lundo la burudani ambazo zina
maswali mengi.
Kwanza
kabisa ni Tanzania kuwa na uhakika wa timu itakayotinga nusu fainali, yaani
timu nne za mwisho.
Ikiwa
Azam au Yanga, moja wapo itakuwa na kazi ya kucheza mechi moja zaidi ili itinge
fainali na baada ya hapo ni ‘mipango’ ya ubingwa.
Kinachovutia
zaidi ni suala la mashabiki wengi wa Simba ambao wamekuwa wakizishangilia kila
timu zinazokutana na Yanga hasa katika michuano ya Kagame.
Mashabiki wengi wa Simba hujitokeza kwa wingi kuizomea Yanga na kumshangilia mpinzani wake.
Lakini
safari hii, Yanga inakutana na Azam FC. Si kwamba ni timu ya Tanzania ndiyo
maana Simba wataishangilia au watahofia kuizomea, lakini hata Azam FC nao
wanaonekana kuwa ‘wasaliti’ kwa Simba.
Hali
hiyo inatokana na ule uamuzi wa mechi ya mwisho ya msimu, wakati Yanga tayari ni
mabingwa na Simba na Azam FC wakiwania nafasi ya pili.
Azam
FC alikuwa na asilimia 75 ya kupata nafasi hiyo huku Simba wakibaki na 25
lakini hawakukata tamaa.
Mechi
iliyokuwa inatakiwa kuamua ni kati ya Yanga dhidi ya Azam FC. Kama Azam
ingefungwa na Yanga, basi ingeibua matumaini ya Simba na ile asilimia 25
ingepanda.
Lakini
Yanga ikalala, Simba wakaona kuwa kulikuwa na ‘mipangp’. Tena wakaalani
kulikuwa na mvua kubwa lakini bado mechi iliendelea kuchezwa kwa kuwa Azam FC
walikuwa wanaongoza na mwisho walishinda.
Kilichowaudhi
zaidi, Simba ambao angalau walionekana na ‘undugu’ na Azam FC kuliko Yanga, ni
kuona Yanga na Azam kwa pamoja wakiwa wameungana na kushangilia mara tu baada
ya mechi.
Mashabiki
wenye njano na kijani, waliunga na wenye nyeupe na bluu na kuangusha bonge la ‘sherehe’
pale Taifa tena bila ya kujali mvua.
Sasa
Simba wataishangilia Azam FC iiue Simba, au kwa mara ya kwanza wataweka rekodi
kuizomea Yanga pamoja na timu wanayocheza nayo.
Je,
ule urafiki wa Yanga na Azam utakuwepo tena Jumatano? Watashangilia pamoja tena
au sana nao ni ‘maadui’?
Hii
ni sehemu ya kuonyesha soka lilivyo na burudani na huenda, Jumatano kutakuwa na
burudani ya kutosha ndani na jukwaani kwenye Uwanja wa Taifa.
0 COMMENTS:
Post a Comment