July 26, 2015

JAMAA AKISAFISHA BAADA YA KUBAMBWA NA WADAU UWANJA WA TAIFA, LEO.Ukishangaa ya Musa, utayaona ya Firauni! Hivi watu bado wanajisaidia haja ndogo kwenye sinki zinazotumika kunawia mikono au uso?


Imetokea leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wakati Yanga ikiivaa Al Kharthoum ya Sudan.

Jamaa mmoja, amewahi kuingia chooni na kwenda kuanza kujisaidia haja ndogo kwenye sinki hizo kwa ajili ya kunawia.
 
Mashabiki walioingia chooni, wakamnasa. Acha wamkomalie, wengine wakitaka kumpiga, wengine watakata kumywesha mkojo wake.

Akionekana amechanganyikiwa, jamaa alianza kujitetea akisema: “mimi nilidhani choo cha wanawake ndiyo wanatumia hivyo.”
 
Jibu lake lilionekana kuwaudhi zaidi wakawa wanataka kumpiga, wengine waliojitokeza na kuwapoza wenzao kuwa na jazba na kuwataka wampe adhabu ya kufanya usafi.

Ndipo aliposimamiwa na kuanza kufanya usajifi wa sinki moja baada ya jingine.

Mtu huyo wa ajabu kabisa aliyewashangaza wengi, alionekana ana umri takribani miaka 45 hivi, lakini anajisaidia kwenye sinki!






0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic